Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo leo Januari 4, 2021 amemtembelea na kumjulia hali mmoja wa waasisi wa Muungano, Mzee Hassan Omar Mzee aliyelazwa katika Kituo cha Afya cha Kibweni Wilaya ya Magharibi ‘A’ Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
Mzee Omar ambaye
alichanganya udongo wakati wa sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Aprili 26, 1964, amelazwa katika kituo hicho cha afya akipatiwa matibabu.
Akiwa katika kituo hicho
Dkt. Jafo aliwashukuru na kuwapongeza wataalamu wa afya katika kituo hicho kwa
huduma wanazotoa kwa Mzee Omar ambaye ni miongoni mwa waasisi muhimu wa
Muungano.
Alisema wataalamu hao
wameonesha uzalendo mkubwa kwa kutoa huduma bora kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi
na waasisi wa Muungano huu adhimu wa Zanzibar.
Pia aliwasihi waendelee na
moyo wa kuwahudumia wananachi wanaofika kupata matibabu kwani kituo hicho cha
afya ni muhimu kwa mustakabali wa afya.
Waziri Jafo yupo Zanzibar kwa
ziara ya kikazi akiwa ameambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya
Makamu wa Rais, Bw. Sigsbert Kavishe, Mkurugenzi Msaidizi wa Muungano kutoka
Ofisi ya Makamu wa Rais – Ofisi ya Zanzibar, Bi. Shumbani Ramadhan na Mratibu
wa Ofisi ya Makamu wa Rais – Zanzibar, Bw. Othman Kassim Haji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Mzee Hassan Omar Mzee (aliyechanganya udongo wa Muungano)
ambaye amelazwa katika Kituo cha Afya cha Kibweni Wilaya ya Magharibi ‘A’ Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar leo Januari 4, 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiagana na maafisa wa Jeshi la Kuzuia
Magendo (KMKM) mara baada ya kumjulia hali Mzee Hassan Omar Mzee (aliyechanganya udongo wa Muungano) ambaye
amelazwa katika Kituo cha Afya cha Kibweni Wilaya ya Magharibi ‘A’ Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar leo Januari 4, 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...