CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), kimeanza mchakato wa kuandikisha wanachama wapya na kuhuisha wanachama wa zamani, ili kuelekea kufanya uchaguzi Mkuu wa kupata viongozi wapya watakaokiongoza chama kwa miaka minne ijayo.
Kutokana na hali hiyo TASWA imepokea maelekezo kutoka Baraza la Michezo nchini (BMT), kuandaa rejesta ya wanachama na kuiwasilisha BMT hadi kufikia Februari 15 mwaka huu, kwa hatua nyingine za kupanga Uchaguzi Mkuu.
TASWA inawaomba wanachama wake wote kuhuisha uanachama wao kwa kulipia ada kuanzia leo Januari 17, 2022 hadi Februari 15, 2022, pia inawahamasisha waandishi wa habari za michezo ambao si wanachama wa TASWA, lakini wanataka kuwa wanachama wajitokeze kuomba uanachama kwa muda huo uliowekwa.
Ili kurahisisha jambo hilo la kuandaa rejesta ya wanachama liwe na ufanisi zaidi, kutakuwa na waratibu wawili, ambao ni Mjumbe wa Kamati ya Katiba ya TASWA, Gift Macha na Mhazini Msaidizi wa TASWA, Zena Chande watakaotekeleza jukumu hilo chini ya usimamizi wa Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando.
Ni matumaini yangu waandishi wengi watashiriki katika jambo hili kwa maendeleo ya chama chetu.
Asanteni
Juma Pinto
Mwenyekiti TASWA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...