Mwito umetolewa kwa waendesha bodaboda katika Wilaya ya Ulanga kufuata sheria za usalama barabarani na kuhakikisha wanaziepuka ajali za uzembe na kumfikisha salama abiria anayetumia usafiri huo
Wito huo umetolewa na wajumbe kamati ya usalama barabarani wilayni ulanga wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani iliyozinduliwa katika kijiwe cha bodaboda kilichopo Togo Mahenge Wilayani Ulanga
Wajumbe hao wamesema kuwa endapo kila mwendesha bodaboda atazingatia na kufuata sheria za barabarani hakutakuwa na ajali katika mji wa mahenge na wilaya kwa ujumla wake hivyo wamewataka bodaboda hao kuzingatia sheria zote za barabarani
Kwa upande wake mkuu wa usalama barabarani JOSEPH SAGALA amesema kuwa kwa mwaka huu wiki ya nenda ka usalama itafanyika kwa kuwatembelea bodaboda kwenye vituo vyao na kuwapatia elimu ya uslama barabarani ili wasio jua sheria wazijue ili kutokomeza ajali za uzembe
Mkuu huyo wa usalama barabarani amesema kuwa wameandaa vyeti vya Madereva bora kwa mwaka huu na watapatiwa vyeti wale madereva wote ambao hajawahi kupata ajali wakati wote wa kazi yao ya bodaboda
Aidha mkuu wa polisi wilayani ulanga JAKSON KAHAMBA amesema ili kutokomeza ajali wilayani ulanga amewataka bodaboda kufika ofisini kwake mara tu wanapoonewa na askari wa usalama barabarani kwani kwa kuhofia kusema ukweli itawapelekea kuzidi kuonewa nayeye asiwe na taarifa ya kuonewa kwao
Mkuu wa Polisi amesema kuwa anasikitishwa na baadhi ya Madereva wa bodaboda ambao wanaonekana kuonewa na hawasemi wanasubiri mpaka kuwe jna mkutano wa hadhara jambo ambalo hajapendezwa nalo
Akihitimisha uzinduzi huo Mwenyekiti wa kamati ya nenda kwa usalama Wilayani Ulanga Bw Christom Msakamba amewataka vijana kuhakikisha ulanga inakuwa haina ajali kwa kufuata sheria za barabarani
Nao bodaboda wameomba uongozi huo kuwapa mafunzo ya mara kwa mara na kusaidia kuwapatia leseni kwa bei nafuu,pamoja na kuahidi kupokea yale waliyopewa na kuyafanyia kazi ili kutokomeza ajali za barabarani za uzembe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...