MWENYEKITI wa Kanisa la Shincheonji Man Hee Lee amesema kanisa hilo linaunga mkono ubadilishanaji wa neno la Biblia kwa kila Kanisa na seminari ulimwengu kote.

Ameeleza hayo wakati wa mkutano maalum na waandishi wa habari kutoka nchi 55 barani Afrika uliofanyika kwa kwa njia ya mtandao na kusema uungaji mkono huo ni kutokana na matokeo chanya yaliyoshuhudiwa na Kanisa la Shincheonji Church of Jesus kupitia unabii na utimizo uliorekodiwa katika kitabu cha Ufunuo kwa ulimwengu kupitia mtandao wa YouTube na tayari Kanisa hilo limetia saini makubaliano na zaidi ya wachungaji na seminari 1,200 katika nchi 57 huku nchi 16 zikiwa za Barani Afrika.

Man Lee ameeleza juu ya maana halisi ya Agano Jipya katika Biblia Ushuhuda juu ya Mafumbo ya Siri za Mbinguni na Maana Zake za Kweli na hiyo ni baada ya matokeo ya semina ya Ufunuo  na semina ya mtandaoni ya Shincheonji.

Katika mkutano huo uliioombwa na vyombo vya habari na wachungaji Barani Afrika na kufanyika mwishoni mwa wiki  Man Hee  amesema washirika hao muhimu ni vyema wakasambaza shuhuda juu ya unabii, utimilifu na Ufunuo wa siri za ufalme wa mbinguni.

"Ushuhuda wa mafumbo ya siri za Mbinguni na maana zake Kweli ni semina ya kufichua mafumbo iliyoanzia kurushwa Januari 3 inaendelea ulimwenguni kote  na inarushwa kupitia chaneli ya YouTube ya Shincheonji kwa lugha 24 tofauti kwa siku za Jumatatu na Alhamis " Amesema.

Aidha alieleza kuwa, anatamani kila mtu ulimwenguni ajifunze neno kutoka semina ya Shincheonji ili kubadilisha maisha yao.




Baadhi ya waandishi wa habari wakiuliza maswali.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...