NA FARIDA SAIDY,MOROGORO 

Baraza la Taifa la  Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limetoa siku tatu kwa dereva wa roli aliye mwaga kemikali ya Sulphur  katika eneo la Msimba Tarafa ya Mikumi Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro kujisalimisha mara moja kutokana na kemikali hiyo kuanza   kuleta madhara kwa wananchi waliokaribu na eneo hilo.

Agizo hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la  Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)  Jamali Baruti ametoa siku hizo baada ya kufika na kujionea namna wananchi wa eneo hilo walivyo athiriwa na Kemikali hiyo.

Imeelezwa kuwa dereva wa lori lililoangusha sumu hiyo iliyokuwa kwenye kontena alitokomea kusikojulikana pamoja na gari yake.

Timu ya wataalamu wa NEMC imefikia hatua hiyo Januari 5 mwaka huu baada ya kupata taarifa ya kutokea kwa tukio hilo huku wananchi wakianza kupata madhara ikiwemo kuumwa  macho ,vichwa kuuma pamoja na kuashwa kwa ngozi.

Hata hivyo kaimu Mkurugenzi wa NEMC amesikitishwa na kitendo cha dereva wa liri hilo aliyekuwa  akitokea Dar es salaam kuelekea nchi jirani ya Kongo kumwaga kemikali ya sulphur na kutokomea kusikojulikana huku ikiwa bado chanzo cha kumwagika kwa sumu hiyo aina ya salfa kikiwa hakijajulikana

Kutokana na hali hiyo NEMC imeanza kumfuatilia na kumchukulia hatua dereva kwa kutofuata sheria ya kuhifadhi mazingira kwani kitendo alichokifanya ni uharibufu wa mazingira huku wahanga wakubwa wakiwa ni wananchi waishio jirani na eneo hilo kwani kemikali hiyo inamadhara makubwa kwa binadamu na mazingira kwa ujumla.

Sambamba na hayo NEMC inatoa rai kwa madereva wanaoendesha magari ya mizigo hususani yanayobeba kemikali kufuata kanuni na miongozo ya ufungaji wa mizigo pamoja na kutumia vifungashio vinavyokidhi vigezo.

Kwa upande wao mashuhuda wa tukio hilo wamesema roli hilo lilidondosha kemikali hizo usiku wa Januari mosi 2022 na kusababisha madhara kwa wananchi ikiwemo kuumwa na kichwa, macho na kifua hali ambayo imeleta sintofahamu kwa wakazi hao kwa kuhofia afya zao.

Aidha walisema ukosefu wa elimu ndio chanzo cha kuathiriwa na kemikali hizo huku wakiiomba Serikali kuwasaidia kupata matibabu ya haraka kunusuru afya zao.

Kemikali ya Sulphur  iliyomwagika katika kijiji cha Msimba Tarafa ya Mikumi Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.

Kaimu Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la  Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)  Jamali Baruti akizungumza na waandishi wa habari katika kijiji cha Msimba ilipomwagika kemikali aina ya Sulphur.

Bwana Daud Mkumbila mmoja wa waathirika wa kemikali ya Sulphur.

Wakazi wa kijiji cha Msimba wakiwa pamoja na maafisa wa NEMC wakiangalia kemikali iliyomwagika pembezoni mwa barabara ya Morogoro­­-Iringa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...