Mbunge wa Mvomero Jonas Van Zeeland akiwa katika pikipiki mara baada ya kukabidhwa vijana pikipiki kama sehemu ya miradi.
Picha mbalimbali za tukio la kukabidhi vijana miradi ya kuendeshea maisha.
*Mbunge Zeeland ampongezs Mh.Rais Samia Hassan Suluhu
Na Mwandishi Wetu
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mvomero imetoa Mikopo kwa vijana ,kina Mama na walemavu zaidi ya Mil 250 kwaajili ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mvomero Mbona Hassan Njama amewataka wale wote waliopewa mikopo hiyo kupitia vikundi vyao kuhakikisha wanasimamia vema miradi yao waliyoibuni Ili kuhakikisha wanarejesha fedha hizo ambazo wakirejesha kwa muda muafaka makundi mengine yatapewa kwani dhamira ya Serikali nikuwakomboa wananchi wake na ndio maana fedha hizo hazina riba yoyote Ili kuwawesesha wananchi wamudu kurudisha.
Hassab amesema fedha ameeleza kuwa wameamua kununua pikipiki na mashine mbalimbali Ili zitumike kwenye vikundi hivyo ikiwa ni sehemu ya miradi yakiubunifu.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero Jonas Van Zeland amempongeza Mh Rais pamoja na Baraza la Madiwani na uongozi mzima wa Wilaya chini ya Mkuu wa Wilaya Halima Okash kwakusimamia vema ila ya CCM pamoja na ukusanyaji wa mapato ambao umepelekea kufikia lengo hilo na wananchi kufanikiwa kupata mikopo hiyo.Mbunge huyo amesema Mh Rais Samia Hassan Suluhu anafanya kazi kubwa kuwatumikia wananchi na hasa wale wa Hali ya chini hivyo anakila sababu ya kuungwa mkono na kila mmoja wetu wakiwemo wote wanaifaidika na fedha hizo.
Mbunge Van Zeeland amesema utoaji wa Mikopo hiyo pongezi za kipekee kwa Baraza la Madiwani chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi Mtendaji kwa kusimamia vyema makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri na kuwezesha Mambo yote haha kufanyika pamoja nimiradi ya Maendeleo kwa fedha za ndani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...