MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Manyara, Kiria Kurian Laizer, ametimiza ahadi yake aliyoitoa hivi karibuni ya kuipatia shule shikizi ya Kandasikira ya Kata ya Shambarai, Wilayani Simanjiro mifuko 100 ya saruji.
Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Simanjiro, Thomas Mollel
akikabidhi mifugo hiyo 100 ya saruji jana kwa niaba ya Kiria
amempongeza kwa kutimiza ahadi yake aliyoitoa hivi karibuni.
Mollel
amesema Kiria aliahidi kutoa mifuko hiyo ya saruji 100 kwa ajili ya
kumalizia madaraja mawili ya shule hiyo shikizi ya Kandasikira, baada ya
ziara ya siku moja ya kamati ya siasa ya CCM ya wilaya hiyo.
Amesema
wadau wengine wanapaswa kumuunga mkono Kiria ili kufanikisha maendeleo
kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ya Simanjiro yenye changamoto
tofauti.
“Ili wanafunzi waweze kusoma vizuri na kufaulu mitihani
yao wanapaswa kusoma katika mazingira bora na yenye kutulia, kupitia
mifuko hiyo 100 yatasaidia kuboresha shule hiyo," amesema Mollel.
Ofisa
mtendaji wa Kijiji cha Kandasikira, Habiba Njau akizungumza wakati
akipokea mifuko hiyo 100 amemshukuru Kiria kwa kujitolea mifuko hiyo ya
saruji.
Njau amesema shule hiyo shikizi inawatoto 400 ina
madarasa sita na wanafunzi wapo kuanzia darasa la kwanza hadi la sita na
mwaka huu wanatarajia kufanya mtihani wa darasa la saba.
“Tunaomba
wadau wengine wa maendeleo waige mfano wa Kiria kwa kuchangia penye
mapungufu ili kuiunga mkono serikali katika kuboresha miundombinu ya
shule," amesema Njau.
Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Wilaya ya
Simanjiro, Innocent Vitalis amesema ameungana na Mwenyekiti wa UVCCM wa
wilaya hiyo kufikisha mifuko hiyo 100 iliyotolewa na Kiria.
Innocent
amesema Kiria alitimiza wajibu wake kwa kukabidhi mifuko hiyo 100 ya
saruji aliyoahidi kutoa baada ya kutembelea eneo hilo hivi karibuni
akiwa na kamati ya siasa ya CCM Wilaya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...