Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde akiwa ameongozana na Diwani wa Kata ya Mkonze Mh. David Bochela wamefanya  ukaguzi wa ujenzi wa daraja kubwa la kivuko katika Mtaa wa Nzinje,Jijini Dodoma.

Daraja hilo ambalo linajengwa chini ya TARURA litakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Mtaa wa Nzinje na maeneo jirani ambao kipindi cha mvua wamekuwa wakipata mkwamo mkubwa wa kuvuka na kuunganishwa na maeneo mengine kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.

Akishukuru kwa niaba,Mbunge Mavunde ameishukuru serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuitengea TARURA fedha za kutosha kugharamia ujenzi wa barabara,mitaro na madaraja Jijini Dodoma hali itakayopelekea maeneo mengi kupitika kwa urahisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...