MKURUGENZI  Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Mhidze (Dkt) amewataka Watumishi wa kada ya afya nchini kuwa Wazalendo na kufanya kazi zao kwa weledi, ili kwa Pamoja kuweza kutimiza adhima ya serikali ya kuboresha afya za wananchi, kupitia miradi mbalimbali ya afya inayoanzishwa nchini.

Meja Jenerali Gabriel Mhidze (Dkt) amesema iwapo kada hiyo ya afya itakubali mabadiliko chanya yanayofanywa na serikali, kutakuwa na ahueni kubwa kwa wananchi, kwani serikali kupitia wizara ya afya imedhamiria kupunguza gharama za matibabu, kuboresha miundombinu ya afya, sambamba na kusogeza huduma mbalimbali za afya karibu na wananchi, ikiwemo huduma ya kusafisha damu kwa wagonjwa figo nchini.

Afande Mhidze ametoa rai hiyo kwenye Hospitali ya jeshi ya Lugalo, wakati akifunga mafunzo maalum ya Kusafisha damu (dialysis), yaliyotolewa kwa watumishi  yaani madaktari, wauuguzi na mhandisi vifaa tiba; kutoka Hospitali  ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala, ili kuwajengea uwezo na umahiri katika kutumia mashine mpya na za kisasa zilizonunuliwa na MSD na zinatarajiwa kusambazwa katika hospitali

Pamoja na rai hiyo, amewatunuku vyeti wahitimu hao na kuwataka kuwa mabalozi wazuri huko waendako, kwa kueneza mazuri waliyojifunza, ili hospitali zingine ziweze kuhamasika na kuanzisha huduma hizo za kibingwa katika maeneno yao.

Dkt. Linda Ezekiel, Mratibu wa  Huduma za magonjwa ya Figo nchini amemshukuru Meja Jenerali Gabriel Mhidze (Dkt), na wadau mbalimbali kwa utayari wao katika kuleta mapinduzi katika matibabu ya kusafisha damu nchini huku akiushukuru uongozi wa Hospitali ya Jeshi Lugalo chini ya Brigedia Jenerali. Dkt.Fredy Kivamba kwa kukubali kuwa mwenyeji mafunzo hayo 

Kwa upande wake Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi, ameelezea uwepo kwa ongezeko kubwa la wagonjwa wenye matatizo ya figo nchini, huku akiwataka wataalamu kufanya kazi zao kwa nidhamu na weledi ili lengo lililokusudiwa na serikali kupitia mafunzo hayo liweze kutimizwa. Sambamba na hilo amewataka wananchi kubadili mitindo hatarishi ya Maisha, ikiwa ni Pamoja na kupima afya zao mara kwa mara  ili kujua yanayowasibu mapema pamoja na kufanya mazoezi.

Wakati Mwakilishi wa wahitimu hao, Dkt.Pantaleo Joseph ameishukuru Serikali kwa kuandaa mafunzo hayo adhimu, na kuupongeza uongozi wa Hospitali  ya Kuu ya Jeshi Lugalo huku wakiomba mafunzo hayo yawe endelevu na yawafikie wenzao walioko katia vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya, kwani yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma na kuokoa Maisha ya wananchi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...