Naibu
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi - Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Godfrey
Kasekenya amezindua mradi wa uimarishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga
nchini tarehe Januari 14, 2022 uliofanyika Makao Makuu ya Usafiri wa
Anga Tanzania jijini Dar es salaam.
Akizungumza katika hafla maalum ya uzinduzi wa mradi huo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Ujenzi - Sekta ya Ujenzi,
Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema fedha hizo zitatumika kuboresha
miundombinu ambayo kwa sasa yanakwenda sambamba na maboresho
yanayofanywa na Serikali katika Shirika la Ndege Nchini.
“Nawapongeza
sana Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), kwa kazi nzuri ambayo
mmeifanya mpaka kuwa miongoni mwa Nchi chache ambazo zimepata fedha
hizo, ni imani yangu kuwa hatutarudi nyuma hasa ukizingatia Serikali
inaboresha Shirika letu la Ndege” amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Bw. Johari Hamza
amesema mradi huo kazi yake kubwa itakuwa ni kuhimarisha Usalama wa
Usafiri wa Anga ili kuweza kupunguza au kumaliza kabisa ajali mbalimbali
pia na uwepo wa watalaamu wa Usafiri wa Anga watakaopata mafunzo
mbalimbali ndani ya mwaka mmoja pamoja na upatikanaji mzuri wa vifaa
bora katika kazi za usalama wa usafiri wa Anga.
Mradi
huo umehudhuriwa na watu mbalimbali mwakilishi wa Balozi wa China
nchini Tanzania Xu Chen, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na
Uchukuzi- Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Ali Possi, Mwakilishi wa Katibu wa
ICAO Barry Kashambo, Wakurugenzi wakuu wa Taasisi pamoja na wadau
mbalimbali wa Sekta ya Usafiri wa Anga Tanzania
Naibu
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi - Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Godfrey
Kasekenya akizungumza kuhusu namna Serikali walivyojipanga kusimamia
Usafiri wa Anga hapa nchini wakati wa uzinduzi wa mradi wa uimalishaji
na udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini uliofanyika tarehe Januari 14,
2022 Makao Makuu ya Usafiri wa Anga Tanzania, Ukonga-Banana jijini Dar
es salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari
akizungumza kuhusu namna Mamlaka hiyo ilivyojipanga kutekeleza mradi wa
uimalishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga wakati wa uzinduzi wa mradi
wa uimalishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini uliofanyika tarehe
Januari 14, 2022 Makao Makuu ya Usafiri wa Anga Tanzania, Ukonga-Banana
jijini Dar es salaam.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi- Sekta ya Uchukuzi, Dkt.
Ali Possi akitoa neno kwenye uzinduzi wa mradi wa uimalishaji na
udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini uliofanyika tarehe Januari 14, 2022
Makao Makuu ya Usafiri wa Anga Tanzania, Ukonga-Banana jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
wa Shirika la Anga Duniani, Kanda ya mashariki na kati (Eastern and
Southern African), Barry Kashambo akizungumza kuhusu namna Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) walivyofanya
kazi kwa bidii na kuitoa Mamlaka hiyo katika asilimia 30 na kufikia
asilimia 67 na kufanya kupata mkopo kutoka katika Shirika hilo uzinduzi
wa mradi wa uimalishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini
uliofanyika tarehe Januari 14, 2022 Makao Makuu ya Usafiri wa Anga
Tanzania, Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam..
Mwakilishi
wa Balozi wa China, Xu Chen akizungumza kuhusu Serikali ya Jamhuri ya
Watu wa China inavyoendelea kutoa misaada kwa nchi zinazoendelea ikiwemo
Tanzania wakati wa uzinduzi
wa mradi wa uimalishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini
uliofanyika tarehe Januari 14, 2022 Makao Makuu ya Usafiri wa Anga
Tanzania, Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) pamoja na wadau mbalimbali wa Usafiri wa Anga wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi - Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya alipokuwa anazindua mradi
wa Uimalishaji na udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini uliofanyika tarehe
Januari 14, 2022 Makao Makuu ya Usafiri wa Anga Tanzania,
Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi - Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Godfrey
Kasekenya akiwa kwenye picha za pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya
Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) pamoja na wadau mbalimbali wa Usafiri wa
Anga mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa mradi wa Uimalishaji na
udhibiti wa Usafiri wa Anga nchini uliofanyika tarehe Januari 14, 2022
Makao Makuu ya Usafiri wa Anga Tanzania, Ukonga-Banana jijini Dar es
Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...