Adeladius Makwega,Dodoma.
Kwa hakika habari kubwa ambayo ilikoza wino katika vyombo vingi vya habari kuufunga 2021 nchini Tanzania ni suala la ukopaji kwa taifa letu huku kukiwa na pande kubwa kubwa mbili, wengine wakisema tukope na wengine wakisema kuwa mikopo ina madhara.
Mjadala ulikuwa dhaifu kwani
ulihamia kumtuhumu mtu binafsi na hata kushambuliana mambo binafsi ambao sioni
kama kulikuwa na tija ya kufika huko.
Hadi saa saba mchana
sikuweza kutatuliwa shida yangu, zaidi ya kupewa namba na kuambiwa kuwa
tunaendelea kulifanyia kazi jambo hilo. Mawasiliano yaliendelea lakini mwisho
wa siku nilijifunza jambo moja kubwa sana maishani mwangu.
Nilitoka hapo hadi Barabara ya Titi Mohammed, kabla sijavuka niwe upande wa Maktaba ya Taifa nilishangaa gari moja ilisimama mbele yangu, jamaa alifunga breki miguuni mwangu,nilishituka kidogo, alinisalimia na kuniuliza Makwega unatokea wapi? Nilimsimulia nilipotoka. Huyu alikuwa jamaa yangu ambaye nilisoma naye siku nyingi. Hivi sasa akihudumu katika taasisi moja kubwa ya dini. Alinipakiza katika gari hilo kwa kuwa kwetu anakufahamu, aliniuliza si unakwenda Mbagala, nilimjibu ndiyo. Tulianza safari ya kuitafuta Mbagala, nikiwa ndani ya gari hilo tuliongea mengi. Nilipomsimulia nilipotoka na kilichonikuta ndugu huyu alinijibu tu.
“Kila jambo lina Arubaini
yake, mimi(yeye) nimekabidhiwa taasisi moja ambaye ina madeni hapa nilipo
natoka kuelezea namna ninakavyolipa madeni hayo ambayo yalikopwa na mtangulizi
wangu.”
Sasa kibaya, hata hiyo miradi inayodaiwa kukopewa haijafanya vizuri, kwa hiyo sasa anajukumu la kulipa huku akitakiwa taasisi hiyo kuweza kusonga mbele na mipango mipya ya maendeleo.
Huku akiniambia kuwa katika hilo wanaweza wakapata 75 ya asilimia ya rejesho angalau kukwepa migogoro ya mashauri kupelekwa katika mahakamani na kufilisiwa, lakini pia kudaiwa huko kunafanya kuzungumzwa vibaya na taasisi za fedha, jambo ambalo linawafanya washindwe kuaminiwa tena. Basi, tuliendelea na safari, tulipofika Mbagala 77 nilishuka na ndugu huyu kuendelea na safari yake kwenda huko Kusini mwa Tanzania.
“La pili Padri Saba alihakikisha baraza linamaliza madeni yote yalikuwa yanadaiwa huku na kule. Nimefika ofisini sikukuta baraza na deni hata la senti tano. Nimekuta amelipa kila kitu, nimefika Julai 10, 2018 vitabu vyote viko vizuri, mahusiano ya kifedha na taasisi za serikali yako vizuri sana. Padri Saba alisafisha mapungufu yetu yote na wahisani wetu wote dunia nzima, mapungufu yaliyokuwepo mpaka tunanyima misaada, alijitosa mtoto wa watu. Padri wetu mpendwa alihakikisha anaweka ripoti zetu vizuri, kuhakikisha anajitoa sadaka, aliweka mahusiano vizuri. Sisi tulipofika, tunapiga hodi tunaambiwa ahaa TEC imejisafisha karibuni sana.” Hiyo ni kazi ya mpendwa wetu Padri Saba.
“Hivyo, hata mahusiano yetu mazuri kwa sasa yanafanya baraza hata katika nyakati hizi ngumu za kiuchumi kutokana na ugonjwa kwa Korona, baraza linaenda. Marehemu hakujua kuwa Korona itakuja kuwa tatizo la uchumi la baraza, lakini kutokana na alivyofanya labda Mungu alimtuma afanye na sasa hivi baraza linaendelea vizuri, kutokana na mahusiano mazuri na wafadhili wetu wa Kikanisa na taasisi zingine.” Aliendelea kuhubiri Padri Kitima.
Ibada hii ilipomaliza nilidoea tena usafiri wa ndugu yangu huyu nayeye kurudi Kusini na mie kushuka zangu Mbagala 77.
Ukiwa umevisoma vizuri visa vyangu vitatu kile cha NMB na mimi mwenyewe, cha huyu ndugu yangu wa Kusini mwa Tanzania na hata hiki cha TEC cha Marehemu Padri Raymond Saba kama kilivyosimuliwa na Padri Charles Kitima inatoa taswira ya taasisi za kifedha zilivyo na pale panapotokea kushindwa kulipa madeni hali inavyokuwa.
Swali ni Je Tanzania itaweza
kufanikiwa kwa kukopa?Au tulipashwa kutazama vyanzo vingine? Je mwezangu
unayesoma matini haya unayo majibu? Mie sina majibu, zaidi ya kuzingoja hizo
arubaini, panapo majaliwa yake Mola. Kwa leo naishia hapo nikiugubiga 2021 na
kuugubua 2022.
0717649257
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...