kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini Dkt.Baghayo Saqware akizungumza wakati alipotelea shirika la Taifa la Bima (NIC) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dk.Elirehema Doriye akizungumza kuhusiana huduma wanazozitoa wakati wa ugeni wa TIRA na IFAD jijini Dar es Salaam.



*IFAD  kushirikiana na NIC na wadau wengine kuangalia sera ya kilimo.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

 SHIRIKA la Taifa la Bima (NIC) kuanza kutekeleza bima ya kilimo na Mifugo ili kufanya wananchi kuwa na maendeleo hata pale panapotokea majanga mbalimbali katika sekta hiyo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kutembelewa na Kamishna wa Bima Nchini Dkt. Baghayo Saqware, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw.Elirehema Doriye amesema ili kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija na kilimo ambacho kinavutia watanzania wengi mojawapo ya vitu vya msingi ni kuhakikisha bima ya kilimo inakuwepo lakini pia sera za kilimo zinaenda kugusa wakulima wadogowadogo na kuhakikisha kwa umoja wao wanaweza wakazalisha.

 Dkt.Elirehema Doriye amesema kuwa shirika hilo litaanza kutoa bima za kilmo kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kilimo Duniani (IFAD) ikiwa ni pamoja na kuangalia sera katika kuanza kutekeleza bima hiyo.

Dk.Doriye amesema katika kuangalia sera hiyo kwa bima pamoja na wadau wengine wakiwemo wizara ya kilimo ambapo baada ya hapo sera hiyo itakuwa imegusa maono ya Rais Samia Hassan  Suluhu ya kutaka kilimo kuwa tija na wakati wa majanga wawe wanaweza kupooza machungu.

Amesema NIC ni kubwa katika utoaji wa bima nchini hivyo lina uwezo wa kutekeleza bima ya kilimo mara baada ya kuangalia sera na kuona namna ya kutekeleza.

Amesema Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini (TIRA) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Kilimo wakiwemo Mfuko wa kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) wamepanga kuanzisha uandaaji wa sera ya Kilimo na mifugo ambayo itaelezea kwa kias kikubwa namna ambavyo wanaweza kutekeleza Bima ya Kilimo na Biima kwaajili ya mifugo.

"Bima ya kilimo kazi yake kubwa ni kuhakikisha inamuondolea hasara ambazo mkulima anawezapata kutokana na majanga mbalimbali kama mvua iliyozidi, wadudu ambao wanashambulia mazao , mvua za mawe, ukame na vitu vyote ambavyo vinaweza kuathiri kilimo na uzalishaji". Amesema Dk.Doriye 

Mwakilishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo Kimataifa (IFAD) Jacqline Machango amesema kuwa wameweka majaribio kwa mikoa minne inayoendesha kilimo cha umwagiliaji ambapo baada hapo watajua namna ya kuangalia sera katika sekta ya kilimo.

Amesema kuwa mikoa ya Majaribio ni Manyara, Singida,Dodoma pamoja na Morogoro ambapo majaribio hayo yameanza kufanyika.

Amesema kuwa katika kutekeleza bima hiyo watatoa ujuzi kwa wadau pamoja na kwenda kujifunza  bima ya kilimo iluvyotekelezwa nchini Uganda.

Machango amesema wameona umuhimu katika suala hilo hivyo wameamua kuweka mkono wao kuona ni namna gani wanaweza kusaidiana na TIRA pamoja na NIC kuandaa Sera hiyo ya Bima pamoja na kuitekeleza kwa kiwango ambacho kinaweza kuonekana kwa kiasi gani sera hii inaweza kufanya kazi.

Kwa upande Kamishina wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware ameiopongeza NIC kwa kazi ambazo wanazifanya hasa kuhakikisha wanamjali mteja kuanzia utoaji huduma pamoja na eneo la utoaji huduma.

Aidha amewataka watumishi wa NIC kuhakikisha wanaendelea kuongeza juhudi katika kazi pia kuhakikisha ofisi zote za shirika hilo zinakuwa vizuri na salama kwaajili ya utoaji huduma kwa Watanzania.

Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Baghayo Saqware akikata utepe wakati wa kufungua ofisi iliyofanyiwa maboresho na NIC jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo Kimataifa (IFAD)  Jacquline Machango akizungumza kuhusiana na IFAD kushirikiana na NIC katika kutoa bima za kilimo ,jijini Dar es Salaam.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...