Makamu Mahonda
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Alhaji Othman Masoud Othman, amewakumbusha waumini wa Dini ya Kiislamu nchini kujitahidi kuendeleza malezi mema ili kusaidia kupata viongozi wema nchini.
Mhe. Othman amayesema hayo leo mara baada ya kukamilika kwa ibada Swala ya Ijumaa katika msikiti wa Ijumaa Mahonda wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja.
Amesema jamii inakabiliwa na changamoto kubwa ya malezi kwa vijana kukosa maadili na kusisitiza kwamba ni vyema kwa waumini kuitumia vizuri neema ya vizazi vinavyopatikana kwa kila mmoja kutimiza wajibu katika kuendeleza malezi mema yanayozingatia misingi na maadili bora ya dini ya Kiislamu.
Amefahamisha kwamba binaadamu wamepewa darja kubwa kutokana na kuomba kupata watoto wanaoweza kuandaliwa kuwa viongozi na wafuasi wema na kuepusha matatizo makubwa yanayoweza kusababishwa na vijana kukosa malezi na maadili kwa mujibu wa miongozo ya uislamu.
Aidha Mhe. Othman ameikumbusha jamii ya Zanzibar kutambua kwamba neema ya kizazi aliyoileta Mwenyezi Mungu hapana budi kwa wazazi na jamii kwa jumla kuendelea kutimiza wajibu wao wa kuwalea vyema kwa kuzingatia maadili ili taifa liweze kuwa na vijanawema wenye maadili yatakayosaidia na kuchangia maendeleo ya taifa.
Mapema Khatib wa swala ya Ijumaa katika Msikiti huo Sheikh Salim Gharib, alikumbusha waumini na viongozi umuhimu kumcha Mwewnyezi Mungu na kutenda haki wanatotekeleza majukumu, wajubu na shughuli zao mbali mbali wanazopewa.
Amesema ni muhimu kwa waumini na viongozi mbali mbali nchini kujitahidi kutekeleza vyema wajibu wao na kuchunga haki kwa mujibu miongozo ya dini na taratibu nyengine mbali mbali zilizopo chini.
Mwisho
Imetolewa na Kitengo cha Habari Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar leo tarehe 07/06/2022.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akitoa salam kwa waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada hya kukamilisha ibada ya swala ya Ijumaa huko Msikiti wa Ijumaa Mahonda wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akitoa salam kwa waumini wa Dini ya Kiislamu ( hawaonekani Pichani) mara baada hya kukamilisha ibada ya swala ya Ijumaa huko Msikiti wa Ijumaa Mahonda wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...