Na John Walter-Babati
WATU wawili wamefariki dunia baada ya pikipiki waliyokuwa wamepanda kugonga lori kwa nyuma lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara kutokana na tairi kupata pancha.

Tukio hilo limetokea barabara kuu ya Arusha-Babati ambapo pikipiki yenye namba za usajili MC. 509 BDK iligongha gari hiyo yenye namba za Usajili T.336 AFE ambayo ni mali ya Siara Laizer.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Banjamin Kuzaga amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Dereva wa pikipiki hiyo Daudi Jumanne (25) mkazi wa kijiji cha Magugu na Hussein Mustapha (21) mkazi wa kijiji cha Kiongozi tukio lililotokea Januari 2,2022 katika kijiji na kata ya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara.

Hata hivyo jeshi la polisi mkoa wa manyara linatoa wito kwa waendesha vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...