Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani ACP Wankyo Nyigesa akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada kukamata mafuta ya Mawese leo Januari 17, 2022 Kibaha Mkoani Pwani.
Madumu yenye yaliyokamatwa yakiwa na mafuta ya Mawese.
Zao la Chikichi kabla halijachakatwa.

Na Khadija Kalili, Kibaha
JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani limewakamata watu wawili kwa tuhuma za kuendesha Kiwanda bubu cha kuchakata mafuta yanayozalishwa kutokana na zao la Chikichi (Mawese).

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani ACP Wankyo Nyigesa alisema kuwa wanamshikilia mtu mmoja aitwaye Halifa Issa dereva mwenye umri wa miaka( 42) kabila Muha mkazi wa Kongowe Wilayani Kibaha amekamatwa akiendesha Kiwanda Cha kuchakata afuta hayo ya Mawese bila ya kuwa na kibali.

RPC Wankyo alisema kuwa Februari 16 mwaka huu majira ya saa saba mchana katika maeneo ya Ungindoni Kata ya Kongowe Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.

"Jeshi la Polisi likiwa katika majukumu yake ya kila siku walimtia mbaroni Halifa Issa mwenye umri wa (42) mfanyabiashara na mkazi wa Kongowe anaendesha Kiwanda Cha kuchakata mafuta ya Mawese pasipo na kibali chochote kutoka serikalinj upelelezi wa tuhuma dhidi ya muhusika. umekamilika na atafikishwa Mahakamani"alisema RPC Wankyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...