WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Eliamani Sedoyeka leo Januari 10, 2022 wameripoti katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ikulu yw Chamwino.
Viongozi hao wamepokelewa na watumishi wa Wizara hiyo wakiongozwa na Naibu Waziri, Mhe. Omari Kipanga na Manaibu Katibu Wakuu, Profesa James Mdoe na Profesa Carolyne Nombo.
Akizungumza na watumishi hao Waziri Mkenda amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuwa wabunifu katika kuwatumikia wananchi pamoja na kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya Elimu.
Naye Katibu Mkuu Profesa Sedoyeka amesema kipaumbele chake ni matumizi ya teknolojia katika Elimu ili kurahisisha upatikanaji wa elimu na kuwataka watumishi hao kushirikiana nae katika kuhakikisha sekta ya elimu, sayansi na teknolojia inaleta matokeo chanya katika uchumi wa nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...