MKUU
wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai ameipongeza benki ya Absa kwa
mchango mkubwa inaotoa katika kuboresha mazingira hapa nchini ikiwemo
mkoani humo.
Kagaigai
ametoa pongezi hizo leo Jumatano wakati akipokea jumla ya miche 2,100
ya miti ya asili kutoka kwa uongozi wa benki hiyo, katika ofisi za Mkuu
wa Mkoa, zilizoko Moshi.
“Kumekuweko
juhudi kubwa zinazolenga kuboresha mazingira mkoani hapa, niwapongeze
kwa mchango wenu huu muhimu na pia nitoe rai kwa taasisi zingine kuiga
mfano wenu”, alisema.
Aidha
aliupongeza uongozi wa benki ya Absa kwa kutoa miche ya miti ya asili
ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa utunzaji wa vyanzo vya maji.
“Mkoa
huu ndiyo nyumbani kwa Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko yote
Barani Afrika, kuendelea kuweko kwake mlima huu ni vyanzo vya maji
vihifadhiwe, hivyo miche ya miti ya asili itachangia katika utunzaji wa
vyanzo hivyo muhimu”, alisema.
“Mlima
Kilimanjaro ndiyo chanzo cha maji ambayo yanatumika kwa maswala
mbalimbali ya kiuchumi kama vile uvuvi, kilimo, mazingira bora na
matumizi aina mbalimbali kwa shughuli zinazofanywa na Binadamu, hivyo
miti ya asili ni muhimu ili vyanzo vizidi kuhifadhiwa”, alisema.
Kagaigai
pia alitoa rai kwa viongozi wa benki hiyo kuutangaza Mkoa wa
Kilimanjaro kama mahali salama kwa uwekezaji ili kuinua hali ya kiuchumi
ya Mkoa huo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya Absa Aron Luhanga,
amesema miche hiyo ya miti ni sehemu ya mchango wa benki hiyo ni sehemu
ya mchango wao kwa jamii kupitia mashindano ya Kilimanjaro Marathon
ambayo Benki ya Absa ibnadhamini kwa mwaka wa tatu sasa.
“Miche
hii ni shukrani zetu kwa uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro
ambao ulisaidia kwa benki yetu kuwa mmoja wa wadhamini wa mbio za
Kilimanjaro Marathon mbazo hufanyika mkoani hapa kila mwaka kwa miaka 20
sasa”, alisema.
Alisema
huu ni msimu wa tatu kwa benki hiyo kushiriki kama wadhamini wenza wa
mbio hizo na kwamba ufadhili huo umechangia kwa benki hiyo kuwa sehemu
ya familia inayochangia maboresho ya sekta ya michezo nchini.
“Leo
tunatoa miche ya miti ya asili 2,100 ambayo inachangia kuhifadhi maji
na hivyo kuchangia uhifadhi wa vyanzo vya maji; tunaahidi kuendelea
kutoa mchango wetu mkubwa katika kuoboresha mazingira mkoani hapa”,
alisema.
Katika
hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa Kagaigai pamoja na Bw. Luhanga wa Absa Bank
waliotesha miti ikiwa ni kumbukumbu ya makabidhiano hayo sambamba na
uzinduzi wa upandaji wa miche hiyo ambayo itapandwa maeneo mbalimbali
mkoani humo kama itakavyoagziwa na uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai (kulia) akipokea moja ya miche
iliyotolewa na Benki ya Absa kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa
benki hiyo, Aron Luhanga (katikati). Kushoto ni Meneja wa Benki ya Absa
Tawi la Moshi Pendo Abdallah.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai akiotesha mti kama ishara ya
kupokea msaada wa miche asili 2100 iliyotolewa na benki ya Absa Mjini
Moshi huku Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano wa Absa Bank, Aron
Luhanga (aliyechuchumaa kulia), Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Moshi,
Pendo Abdallah (kushoto) na Afisa Mauzo, Baraka Haule.Hafla hiyo
ilifanyika katika ofisi na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai (kulia) akishuhudia Mkuu wa
Masoko na Mahusiano wa Absa Bank Aron Luhanga akiotesha mti kama ishara
ya makavbidhiano ya miche 2100 iliyotolewa na benki hiyo kwa mkoa wa
Kilimanjaro. Wengine kutoka kulia ni Meneja wa Absa Tawi la Moshi, Pendo
Abdallah na Afisa Mauzo Saidi Borakupata.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...