Na Said Mwishehe, Michuzi TV
SHIRIKISHO
la Vyama vya Magonjwa Yasioambukiza Tanzania (TANCDA) limesema
limeridhishwa na majadiliano,moani ,ushauri na mapendekezo yaliyotolewa
na wadau mbalimbali wakiwemo wabunge katika kuangalia nini kifanyike
kushiriki magonjwa yasiyoambikiza ambayo yamekuwa tishio nchini.
TACDA
kwa kushirikiana na Wizara ya Afya iliona haja ya kuandaa mkutano na
wadau hao kwa lengo la kuwasilishwa muhtarsari wa sera mbalimbali kuhusu
lishe na ufanyaji mazoezi.
Akizungumza
kuhusu mkutano huo Meneja Mirado wa TANCDA Happy. Nchimbi amesema
wameridhishwa na washiriki wa mkutano huo kwani matarajio yao yamefikiwa
kutokana na kupokea maoni na ushauri ambao watafanyia kazi.
"Ndicho
tulichokuwa tunatarajia kikubwa ilikuwa nikuwasilisha muhtarsari wa
sera mbalimbali juu ya lishe na ufanyaji mazoezi na yamepokelewa vizuri
na maoni na ushauri yamekuwa mazuri ,hata waheshimiwa wabunge wamepokea
na wameonesha watafanyia kazi.
"Lakini
katika mkutano huu tulikuwa na Mkurugenzi wa Magonjwa Yasioambukiza
kutoka Wizara ya Afya ambaye naye kwa pamoja kupitia sera ambazo
zimewasilishwa juzi na jana ametoa agizo na ametoa mapendekezo ya
kuanzisha kampeni ya pamoja ya kupambana na magonjwa yasiyoambikiza
ambayo na sisi tunaahidi kushirikiana na Serikali kuhakikisha kwamba
tunafanikisha hilo,"amesema Nchimbi.
Katika mkutano huo wadau Wengine walishiriki ni Chama cha
wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA) maofisa wa Wizara ya Afya
kupitia
Mradi wa RECAP unaosimamiwa pia na shirika la afya Duniani, waandishi
wa vyombo vya habari pamoja na mashirika na Taasisi za umma na binafsi.
Aidha
katika mkutano huo, Mbunge wa Jimbo la Malinyi mkoani Morogoro Antipas
Mgungusi ... ametumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa TANCDA kwa
kuwashirikisha waandishi kutoka vyombo na kwamba wakiwa sehemu ya
majadiliano na kampeni zinazoendelea kuhusu kudhibiti magonjwa
yasiyoambikiza itakuwa rahisi jamii ya Watanzania kupata taarifa sahihi
kuhusu harakati hizo .
"Uwepo
wa waandishi hapa ni muhimu sana, tunafahamu tutaweka mipango lakini
ili wananchi wajue lazima waandishi wa habari watoe taarifa,katika
mkutano huu wameshirikishwa ,hili ni jambo la kupongeza,"amesema
Mgungusi huku akitoa rai pia kwa wanawake nchini kuwa mstari wa mbele
katika kuzikinga familia dhidi ya magonjwa yasiyoambikiza kwa kuandaa
mlo bora kwani magonjwa hayo yanatokana na mtindo mbaya wa maisha
ikiwemo ulaji vyakula.
Meneja Miradi wa TANCDA Happy Nchimbi (aliyesimama)akifurahia na washiriki wa mkutano huoMbunge wa Jimbo la Malinyi mkoani Morogoro Antipas Mgungusi akichangia wakati wa mkutano huo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...