Na Mwandishi Wetu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi ( pichani) akichangia na kutolea ufafanuzi masuala kadhaa wakati wa majadiliano ya mada iliyohusu dhana ya mgawanyo wa madaraka, na namna ya kudhibiti muingiliano wa madaraka ya mihimili ya dola.
Mada hiyo iliwasilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Jumanne Sagini ( Mb) katika siku ya tatu ya mafunzo yanayotolewa kwa Kamati ya Uongozi ya Bunge, Makamu Wenyeviti wa Kamati na wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge.
Baadhi ya masuala aliyoyatolewa ufafanuzi Mwanasheria Mkuu wakati wa majadiliano hayo, ni pamoja na, utaratibu wa kinidhamu kwa majaji, utaratibu wa viapo kama ulivyowekwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Viapo sura ya 266.
Pia alitolea ufafanuzi kuhusu sheria zingine na hujuma wanazofanyiwa wabunge na mamlaka zingine majimboni.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeandaa mafunzo hayo ya wiki moja ya kuwajengea uwezo viongozi wa Bunge na yanafanyika katika Ofisi Ndogo ya Bunge Visiwani Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...