Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wananchi wa kijiji cha Ibumila kata ya Igongolo wilayani Njombe wameishukuru serikali kupitia shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Njombe kwa kuwatoa kwenye giza mara baada ya kufikisha huduma ya umeme katika kaya zaidi ya 80 kwa siku moja katika kijiji chao.

Frolida Mhema na Godern Mhema na miongoni mwa wakazi wa kitongoji cha Magereza katika kijiji hicho,wamesema kwa muda mrefu walikuwa wakihitaji huduma hiyo kutokana na kuishi kwenye kiza nyakati za usiku huku pia wakirudi nyuma kimaendeleo kutokana na kufuata mbali huduma za umeme ikiwemo kusaga na kukoboa nafaka jambo ambalo lilikuwa linawapotezea muda.

“Umeme huu tuliusubiri kwa hamu na tunashukuru kwa kuona umekuja,kwa kweli biashara hapa zilikuwa chini kwa hiyo Mungu ametusaidia na tunaishukuru serikali yetu,ninaomba pia TANESCO waongeze jududi ili na wenzetu walau wapate”alisema Frolida Mhema

Godern amesema “Tungeomba pia watupunguzie changamoto ya kukatika kwa umeme ili kusudi ila kwasasa tunashukuru sana kwasababu leo tumefikishiwa kwa ghalama naafuu”

Kaimu meneja wa TANESCO Njombe, Mhandisi Yusuf Omary Salim amesema mradi huo umegharimu zaidi ya TSh million 80 na tayari wateja zaidi ya 80 wameshaunganishwa na huduma hiyo.

“Hapa kijiji cha Ibumila tulikuwa na mradi wa zaidi ya KM 3 na zaidi ya milioni 80 zimetumika kwenye kujenga mradi na leo tumewaunganishia zaidi ya wateja 80 amabao wamelipia shilingi 27,000”alisema Mhandisi Yusuph

Aidha, amewataka wananchi kuwa makini kwasababu umeme ni hatari pia kama ikitokea kuna shida labda nyaya zimedondoka wawasiliane na shirika hilo.

“Kwanza huu ni mwanzo na lengo letu ni kuhakikisha tumewaunganishia wateja wote na leo hapa tuko kama timu tuna zaidi ya magenge 15 tunapenda pia kuwahamasisha wananchi sasa waweze kulipia kwa wingi ili waweze kupata umeme”alisema Yusuph

Shirika hilo linaendelea na zoezi la kuwaunganishia wateja wake umeme kupitia kampeni ya ''tumejipanga,kutana na TANESCO nyumbani kwako'' inayotekelezwa mkoani humo kuhakikisha wateja wote waliolipia wanapata umeme katika kipindi cha mwezi mmoja.

Fundi kutoka shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Njombe akiendelea na zoezi la kuunganisha umeme kwenye moja ya nyumba iliyopo kitongoji cha Magereza.
Kaimu meneja wa TANESCO Njombe, Mhandisi Yusuf Omary Salim akieleza namna shirika hilo linavyoendelea na zoezi la kuunganisha umeme katika kijiji cha Ibumila.
:Gari ya mafundi kutoka TANESCO ikisambaza nyaya na nguzo za umeme kwenye nyumba zinazopaswa kuunganishiwa umeme.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...