Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi, Stephen Adili akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Elimu ya Fedha kwa Wamachinga iliyoendeshwa na Benki ya CRDB leo tarehe 20/02/2022 katika ukumbi wa PTA Sabasaba. Mafunzo haya yamehudhuriwa na Shirikisho la Umoja wa Wamachinga mkoa wa Dar es salaam (Machinga Saccos) na baadhi ya wawakilishi wa wafanyabiashara hao kutoka Mikoa yote Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa ushirikiano tulionao kati ya Benki yetu na wafanyabiashara wadogo (Wamachinga).
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Elimu ya Fedha kwa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga mkoa wa Dar es salaam lililoendeshwa na Benki ya CRDB leo tarehe 20/02/2022 katika
ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga mkoa wa Dar es salaam, Steven Lusinde akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Elimu ya Fedha kwa
Shirikisho la Wamachinga mkoa wa Dar es salaam lililoendeshwa na Benki ya CRDB leo tarehe 20/02/2022 katika
ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...