Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu imemkuta na kesi ya kujibu, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu katika mashitaka 5 kati ya 6 hivyo wanapaswa kuanza kujitetea.

Uamuzi huo umetolewa leo Februari 18 na Jaji Joachim Tiganga ambapo amesema Mahakama imepitia ushahidi wote wa Mashahidi 13 wa upande wa Jamuhuri ambao umewafanya Washitakiwa wakutwe na kesi ya kujibu.

Hata hivyo Mahakama hiyo imemuachia huru Mshtakiwa wa kwanza baada ya kutokuwa na kesi ya kujibu katika shitaka la sita la kukutwa na sare na vifaa vya Jeshi licha ya kwamba atajitetea katika makosa mengine.

Hata hivyo, mahakama imeona mshtakiwa wa kwanza Khalfan Bwire . hana kesi ya kujibu katika shtaka la kukutwa na sare za jeshi la wananchi na hivyo imemuachia huru katika kosa hilo .


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...