Na. Majid Abdulkarim, WAF- DODOMA

Chama Cha Madaktarai Wanawake (MEWATA) wametakiwa kuimarisha ushirikiano kwa kuhamasisha na kuelimisha jamii kupata chanjo ya Uviko-19 pamoja na kuwandaa wananchi kupokea, kukubaliana na mabadiliko ya hali yoyote ya afya yanayojitokeza Duniani.

Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawakena Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 19 wa MEWATA, unaongozwa na kauli mbiu “Kuimarisha uchanjaji wa Chanjo dhidi ya UVIKO-19 miongoni mwa Madaktari Wanawake Tanzania”.

Waziri Gwajima amesema mkutano huo umefanyika muda muafaka, kwa kuwa mpaka sasa bado Dunia inaendelea kutekeleza jitihada mbalimbali za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa virus vya Corona ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya watu ulimwenguni.

“MEWATA juhudi za kukabiliana na UVIKO-19 zinahusisha wadau mbalimbali wakiwemo wanawake na nafasi yetu katika jamii kwa mantiki hii, ushirikiano wa wataalamu wa sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii hususan wataalamu wanawake kuwa mstari wa mbele itaongeza tija Zaidi”. Ameeleza Dkt. Gwajima.

Vile vile Dkt. Gwajima amebainisha kuwa MEWATA yenye wataalamu wanawake ikishirikiana na wizara ya maendeleo ya jamii itaweza kufikisha ujumbe wake kwenye jamii kwa ufanisi zaidi na siyo tu kwa UVIKO -19 bali hata kwa mambo mengine yanayohusu changamoto za afya ili jamii ielewe kwa lugha nyepesi zaidi ya wataalamu wa maendeleo na ustawi wa jamii walioshirikiana na MEWATA

“Ninatambua kuwa bado kuna wananchi wengi ambao bado hawajapata elimu ya kutosha ya CHANJO ya UVIKO-19 pamoja na elimu juu ya masuala mengine ya afya tuendelee kushirikiana na kuwafikia kwa kuwapa elimu ya kutosha kuhusu chanjo na ugonjwa wa UVIKO-19 kwa ujumla pamoja na elimu ya afya juu ya magonjwa mbalimbali na mila potofu za jamii zinazopelekea kuathiri afya hasa kwa watoto na wanawake”, amesisitiza DKt. Gwajima

Dkt. Gwajima amesema kwa MEWATA ambao tayari wamepata elimu ya kutosha na kuchanja na kwa nafasi zao kama wataalmu wanawake, amewataka kuwa mabalozi wazuri wa kuhakikiksha kuwa mnaendeleza jitihada za kuwafikisha elimu hii wale ambao bado hawajafikiwa hususan wanawake ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya kujikinga kwa kupata chanjo ya UVIKO 19 wao na familia zao.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya TAMISEMI, Dkt. Grace Magembe amesema kuwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuboresha sekta ya afya na kuipa kipaumbele katika maswala ya lishe,afya tiba, afya kinga na eneo la mama na mtoto.

“Sisi kama Madaktari Wanawake Tanzania tunajukumu kubwa la kutoa elimu kwa jamii kwa maana ya kubadilisha fikra potofu na kuwafikishia huduma bora wananchi”, amesisitiza Dkt. Magembe

Naye Rais wa MEWATA Dkt. Mary Charles ameeleza lengo kuu la mkutano huo kuwa ni kuhamasisha Madaktari Wanawake kuwa mabalozi kwa wananchi juu ya kupata chanjo ya Uviko 19.
Dkt. Mary amesema kuwa pia mkutano huo unalenga kutatua changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wa kutekeleza majukumu yao.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...