Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dar es Salaam

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Leah Kihimbi Februari 25, 2022 ametembelea hoteli ya APC iliyopo Mbweni jijini Dar es Salaam ambapo wasanii mbalimbali watakaotumbuiza na kulipamba Tamasha la Serengeti watapiga kambi hivi karibuni kujifua kuelekea tamasha hilo litakalofanyika Machi 12, 2022 jijini Dodoma.

Tamasha hilo ni la watanzania wote huku wasanii mbalimbali wa kizazi kipya na nguli wa muziki nchini watatumia fursa ya jukwaa hilo kuonesha vipaji vyao na kuwapa burudani wananchi wa Dodoma na dunia kushuhudia vipaji vya muziki mubashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari zikiwemo redio, TV na mitandao ya kijamii.

Akizungumza na maelfu ya wageni mbalimbali waliohudhuria tamasha la kimataifa la Sauti za Busara Zanzibar Februari 14, 2022, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa aliwakaribisha wageni kutoka sehemu mbalimbali duniani kushiriki kwenye tamasha la kihistoria la muziki la Serengeti litakalofikia kilele chake Machi 12, mwaka huu jijini Dodoma.

Tamasha hilo limezinduliwa Februari 11, 2022 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi ambapo alibainisha kuwa Tamasha hilo litakuwa bora na la kihistoria ambalo takribani wasanii 50 watatumbuiza katika tamsha hilo. 

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Leah Kihimbi (aliyevaa gauni la pinki) Februari 25, 2022 ametembelea hoteli ya APC iliyopo Mbweni jijini Dar es Salaam ambapo wasanii mbalimbali watakaotumbuiza na kulipamba Tamasha la Serengeti watapiga kambi hivi karibuni kujifua kuelekea tamasha hilo litakalofanyika Machi 12, 2022 jijini Dodoma.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...