Na Amiri Kilagalila,Njombe
Chama
cha wanasheria wa Tanganyika TLS mkoa wa Njombe kimesema tangu kuanza
kwa ugonjwa wa Uviko 19 mawakili 65 nchini wamefariki dunia pamoja na
kuathiri hali ya kiuchumi.
Hayo
yameelezwa na mratibu wa chama cha wanasheria Tanganyika TLS mkoa wa
Njombe Innocent Kibadu katika maadhimisho ya siku ya sheria
yaliyofanyika viwanja wa mahakama ambapo alisema athari za uviko
hazikuishia tu kuchukua maisha ya wapendwa wao bali tu imeathiri kwa
kiasi kikubwa hali ya kiuchumi kwa mawakili binafsi na familia zao.
"Athari
za uviko 19 ni nyingi ikiwa ni pamoja na watu kupoteza
maisha,kudhoofika mwili,kupunguza kasi ya kufanya kazi, kuathiri uwezo
wa taasisi mbalimbali zinazojitegeme na za umma kujiendesha kiufanisi na
kurudisha nyuma mipango ambayo kila taasisi imejiwekea"alisema Kibadu.
Kibadu aliongeza kuwa"sisi kama chama tumepoteza jumla ya mawakili wenzetu wapatao 65"alisema.
Akizungumza
kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya,mkuu wa wilaya ya
Njombe Kissa Kasongwa alisema jamii inapaswa kujitokeza kupata chanjo ya
Uviko 19 kwa sababu ni salama kwa binadamu.
"Chanjo
ipo kwenye vituo vyote vya kutokea huduma,chanjo hii ni salama nendeni
mkachanje ili muweze kuwa salama"alisema Kasongwa.
Naye
hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Njombe Liadi Chamshama
amesema kuwa uanzishwaji wa mahakama ya kimtandao itasaidia kupunguza
mrundikano wa mashauri mahakamani.
"Licha
ya kupunguza mrundikano wa watu pia itasaidia ufanisi na kupunguza
uwapo wa mashauri mengi yanayoletwa mahakamani kwa mujibu wa
sheria"alisema Chamshama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...