Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza na ujumbe wa wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia (walioko kushoto) wanaotembelea Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji.


Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini (katikati) katika kikao na Wawekezaji kutoka nchini Saudi Arabia(hawapo pichani) kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Hemedi Mgaza na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi Balozi Edwin Rutageruka wakati wa kikao na wawkezaji hao


Waziri Mulamula (katikati) katika picha ya pamoja na ujumbe wa wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia waliokuja nchini kuangalia fursa za biashara na uwekezaji baada ya kumalizika kwa kikao chao jijini Dodoma

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Ali Mwadini akiwa nje ya jengo la Wizara katika Mji wa Serikali Mtumba akizungumza na wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia aliokuja nao Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji baada ya kumalizika kwa kikao chao na Mhe Waziri Mulamulajijini Dodoma





Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia wanaotembelea Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji.

Mhe. Waziri Mulamula amekutana na Ujumbe wa wawekezaji hao ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma leo tarehe 02 February 2022. Ujumbe wa wawekezaji hao umeongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudia Arabia Mhe. Ali Mwadini umeelezea utayari wao wa kuja kuwekeza nchini.

Akizungumza katika kikao hicho Balozi Mulamula amewakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikishia mazingira rafiki ya uwekezaji nchini na kwamba Tanzania iko tayari kuwapokea.

Amesema Tanzania na Saudia zina uhusiano wa muda mrefu ambao una historia ya aina yake na kwamba uwekezaji kutoka kwa kampuni hiyo ni sehemu ya kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia.

Kampuni hiyo inayomiliki viwanda mbalimbali nchini Saudi Arabia inajishughulisha na uzalishaji wa pembejeo za Killimo hususan, mbolea za kupandia na kukuzia mimea pamoja na dawa (pesticides) aina ya ‘phosphorus, nitrogen, potassium na sulfur’.

Mbali na uzalishaji wa mbolea na dawa, Kampuni hiyo pia inazalisha vifaa vya kilimo vya plastiki ikiwa ni pamoja na khusambaza bidhaa katika nchini za Saudi Arabia, ukanda wa Mashariki ya Kati na duniani kote.

Wawekezaji hao waliwasili nchini Januari 28, 2022 wametembelea Mikoa ya Mtwara, Lindi Mtwara na Dodoma na kukutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Mikoa hiyo, wadau wa sekta binafsi na wakulima wa korosho kuzungumzia biashara na uwekezaji katika nyanja hizo.

Wawekezaji hao wamemuhakikishia Mhe. Waziri Mulamula juu ya nia yao ya kuja kuwekeza Tanzania na kutaja maeneo ambayo ni kipaumbele chao kuwa ni madini, biashara, kilimo na mifugo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akizungumza na ujumbe wa wawekezaji kutoka Kiwanda cha Pioneers Chemical Factory cha nchini Saudi Arabia wanaotembelea Tanzania kuangalia fursa za biashara na uwekezaji.Kikao hicho kilifanyika ofisini kwa Mhe. Waziri Mttumba jijini Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...