Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Hamis Amiri akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, kuhusu maendeleo ya upanuzi wa kiwanja cha Ndege cha Arusha wakati alipotembelea na kukagua mradi wa huo, Mkoani Arusha.

Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Arusha, Elipid Tesha akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, eneo la mradi wa ujenzi wa sehemu ya maegesho ya ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Arusha, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea kiwanja hicho mkoani Arusha. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa eneo la maegesho ya ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Arusha. Mradi huo umegharimu takribani Shilingi bilioni 1.9 na unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba 2022.

Meneja kiwanja cha Ndege cha Arusha, Elipid Tesha akimuonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, ramani ya jengo la abiria ambalo litajengwa katika Kiwanja cha Ndege cha Arusha, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea kiwanja hicho mkoani Arusha. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) HAmis Amiri

(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi)


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...