Na.Khadija Seif, Michuzi TV
MWANAMUZIKI Mkongwe wa Kitanzania anaeishi nchini China Fresh Jumbe akizungumza na waandishi Wahabari jijini Dar es salaam febuari 20 mwaka huu , Mara baada ya kueleza dhamira yake ya kuwekeza katika Sekta ya Afya nchini Kwa kuletea vifaa vya kisasa vya kupima magonjwa mbalimbali .
Jumbe ambaye amewahi kutesa na vibao mbalimbali ikiwemo 'Mazingira Yetu' ametambulisha kampuni ya uwekezaji wa vifaa akiwa na lengo la kusaidia nchi yake.
Msanii huyo amesema kutokana na uwekezaji huo hivi sasa maisha yake muda mrefu yatakuwa Tanzania huku akieleza kuwa anaanza na sekta ya afya na baadaye atajikita kwenye Muziki ambapo ana mpango wa kuleta studio ambayo itawasaidia wanamuziki kurekodi wimbo wa kisasa wa dansi na taarabu zitakazouzika kimataifa.
Katika uwekezji huo, amesema kampuni itauza vifaa ambavyo ni 'used' na vipya zikwemo mashine za X-Ray, MRI na vingine.
"Tumeamua kampuni itauza vifaa ambavyo vimetumika na vipya, hivyo watakaokuwa na uwezo wa kununua vipya watavipata na wale ambao wanataka vya bei nafuu pia watavipata na ni vile ambavyo vilishatumika,"amesema Jumbe.
Hata hivyo ameweka wazi sababu za kuwekeza kwenye sekta ya afya ni kutokana na kuona wataalamu kwa sasa kwa kiasi fulani wapo wengi ila tatizo lipo katika vifaa, hivyo kwa uwekezaji huo anaona kuwa ataokoa wananchi wengi.
MWANAMUZIKI Mkongwe wa Kitanzania anaefanya vizuri katika anga ya muziki nchini china Fresh Jumbe akizungumza na waandishi Wa habari jijini Dar es salaam, mara baada ya kueleza dhamira yake ya kuwekeza katika Sekta ya Afya nchini Kwa kuletea vifaa vya kisasa vya kupima magonjwa mbalimbali ambapo Kampuni yake itauza vifaa hivyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...