Kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd Imeingia mkataba na serilkali wa kusambaza vifaa vya miradi ya maji ikiwa ni jitihada za serikali  kuhakikisha inamaliza tatizo la maji mijini na vijijini

Akizungumza wakati wa kusaini mikataba hiyo Katibu mkuu Wizara ya Maji nchini Mhandisi Anthon Sanga aliwataka walioshinda tenda hizo za 'kusuply'  vifaa hivyo kuhakikisha wanakamilisha na kukabidhi kwa wakati na isizidi mwezi wa tano ili kuendana na kasi ya Rais Mhe.Samia Suluhu Hassani ya kuhakikisha miradi inamalizika kwa wakati

Kwa upande wake Mkurugezi wa Kampuni ya GF Trucks & Equipments Ltd Imrani Karmali alisema wao wamelipokea agizo hilo la kukamilisha na kukabidhi vifaa hivyo kwa wakati

Pia aliishukuru Serikali kwa kuaminiwa na kwamba wao kama Kampuni hawataingusha katika hilo na ikiwezekana kabla ya mwezi wa tano kila kitu kitakuwa tayari,Ikizingatiwa kuwa  GF inayomiliki kiwanda cha kutengeneza Magari hapa hapa nchini Tanzani kilichopo Kibaha mkoani Pwani

Mwisho kupitia miradi ya maji wao itakuwa kazi nyepesi kwao kwani kupata kwa tenda hiyo kutaongeza Tija katika kiwanda chao na kwa kuwa wana wataalamu wa Kitanzania itakuwa rahis kukamilisha mahitaji kwa wakati

Mkurugenzi wa kampuni ya GF Trucks Equipment’s Ltd ,Imran Karmali(kulia) na Katibu mkuu Wizara ya maji Eng Anthon Sanga wakisaini mkataba wa kusambaza  vifaa kwa ajili ya miradi ya maji uliofanyika jijini Dodoma.Picha na Said Khamis


Mkurugenzi wa Bing Bang akibadilishana nyaraka na Katibu mkuu Wizara ya maji Eng Anthon Sanga wakati wa hafla ya kusainin mikatyaba na makampuni ya kusuply vifaa katika miradi ya maji nchini


Mkurugenzi wa kampuni ya GF Trucks Equipment’s Ltd ,Imran Karmali(kulia) na Katibu mkuu Wizara ya maji Eng Anthon Sanga wakionesha mikataba baada ya kusaini kwa ajili ya kusambaza  vifaa vya miradi ya maji mipya nchini wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dodoma.Picha na Said Khamis



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...