Simba uso Kwa uso na Mimosas Kwa Mkapa

   Na.Khadija Seif, Michuzi TV

KAMPUNI ya Startimes Tanzania, imetangaza kurusha  moja kwa moja (Live) Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kwa hatua za makundi, inayoanza kutimua vumbi Februari 12.       

Akizungumza na waandishi Wahabari Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui David Malisa,  alisema kuwa lengo la Star Times kurusha michuano hiyo ni kujali Watanzania wapendwa michezo.   


"Leo tutafanya uzinduzi huu wa Michuano ya Mpira wa miguu wa Federation Cup (kombe la shirikisho Afrika) kupitia kisimbuzi cha startimes".   

"Kwakuwa Startimes tunawajali wateja wetu wasipitwe na mambo mazuri, tunazidi kuwapa burudani mara 100 zaidi kama kampeni yetu ya mwaka huu inavyosema, kwa mara ya kwanza tunawaletea Michuano hii ya kombe la shirikisho Afrika ambayo itaanza kuonekana rasmi kuanzia siku ya Jumapili"amesema Malisa.                         

Malisa ameongeza kuwa  habari nzuri zaidi ni kwamba Michuano hiyo itaonyeshwa Mubashara kupitia Chaneli ya TV3 tena kwa lugha ya Kiswahili.          

"Kwa watumiaji wa Dish chaneli ya TV3 inapatikana kupitia chaneli namba 197 na kwa watumiaji wa Antenna kupitia chaneli namba 131, Ninachowasishi watazamaji wetu na wateja wetu wapendwa ni kulipia kifurushi cha Smart (Dish)kwa shilingi 21,000 tu mwezi mzima ama kwa watumiaji wa Antenna kulipia kifurushi cha Mambo kwa shilingi 15,000 tu mwezi m zima ili uone LIVE michuano hii hasa chama la wana Simba wakijitutumua. Hii ni nafasi kwako wewe kujiunga na familia ya StarTimes ili uweze kufurahia vipindi bora, chaneli bora kwa vifurushi vya gharama nafuu kabisa". 

Pia amesema katika Michuano hiyo itakuwa na Wadau mbalimbali wa Michezo  Antonio Nugaz, ambaye atakuwa sehemu ya uchambuzi.                

Akizungumzia michuano hiyo Mkurugenzi wa TV3 Ramadhan Msemo, amesema kuwa wapenzi wa soka nchini watarajie mambo mazuri, maana wataonyesha mechi zote za michuano hiyo. 

" Tanzania imepata bahati kuwa na mwakilishi ambaye ni Klabu ya Wekundu wa Msimbazi (Simba, )ambapo Jumapili itacheza mechi yake ya kwanza ya hatua hiyo dhidi ya Asec Mimosas utakaofanyika kwenye Uwanja wa Mpaka Jijini Dar es Salaam."

Mwanafamilia mpya wa "Startimes" Antonio Nugaz akizungumza na waandishi Wahabari na kutoa Amsha amsha mara baada ya kutangaza rasmi Michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika kuruka Mubashara tv3 kupitia Kisimbuzi Cha Startimes

Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malissa akifafanua zaidi kuwa Lengo la Startimes ni kuleta burudani mara 100 zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...