Na.Vero Ignatus,Arusha.
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama,kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia jan 2021-jan 2022 imeweza kukamata kiasi cha dawa za kulevya kutoka nje ya nchi kiasi cha kg 950.8 sambamba na kuangamiza mashamba ya mirungi hekari 10.5,kilo 861 zimeweza kupatikana kutokana na oparesheni iliyofanyika ya kuteketeza hekari 10 za bangi, zaidi ya watuhumiwa 500 walikamatwa.
Hayo yamesemwa jana 15 feb 2022 na Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo Gerald Musabila Kusaya katika mkutano wa uhamasishaji wa mradi wa upunguzaji wa madhara kwa watumiaji wa dawa za kulevya mkoani Arusha kwamba dawa zinazosumbua sana hapa nchini ni pamoja na bangi na mirungi ambapo ambapo amesema wanaendelea kutoa elimu kuanzia shule za msingi na jamii kwa ujumla lengo likiwa ni kila mmoja kupata ufahamu na kuchukia dawa hizo vita hiyo wataikamilisha ndani ya kipindi kifupi
Dawa tulizozikamata zinajumuisha heroin na Methaphetamine na ndiyo maana utakuta sasa katika hilo jumuiso lake la kilo 950.8,kilo 550.2 ni hiyo ni dawa aina ya heroin,ambapo kilo 400.ni Methaphetamine,kwahiyo sasa katika vipindi vyote vilivyopita zimekamatwa aina hizo mbili za dawa za kulevya.alisema Kusaya
Kusaya amesema kwamba dawa yeyote ya kulevya inaathiri ubongo ,akili,hivyo matumizi ya dawa hizo ni chanzo kimojawapo cha kupunguza nguvu kazi ya Taifa kuongeza umasikini kwa familia,ambapo biashara hiyo husababisha mzunguko wa fedha haramu,mfumuko wa bei,utakatishaji fedha,kukithiri kwa rushwa na kuongeza tofauti ya kipato,ambapo serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa kudhibiti tatizo la dawa za kulevya kwenye ukamataji pamoja na matibabu,kwani asilimia kubwa ya vijana ndiyo waathirika wakuu.
Amesema kuwa katika kuonyesha jidihada za mapambano Dhidi ya dawa za kulevya na sambamba na udhibiti wa kemikali bashirifu Tanzania imeteuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa nchi kiongozi katika mapambano ya dawa za kulevya,katika ripoti ya mwisho iliyofanywa na Umoja huo iliweza kuipa nchi asilimia 90% .
‘’Tumejitahidi kama Mamlaka kuhakikisha kwamba mianya ya kuingiza dawa za kulevya tunaidhibiti na tumefanya vizuri,ila tatizo limebakia hapa nchini kwenye udhibiti wa bangi na mirungi, asilimia kubwa ya vijana ndiyo waathirika wakuu,Kiafya dawa hizo za kulevya zimekuwa zikisababisha magonjwa ya moyo,ini ,mapafu,meno,ngozi,figo na sarartani,ambapo mazingira duni ya kujidunga huongeza maambukizi ya vvu na homa ya Ini’’.alisema .
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela katika ufunguzi wa kikao kazi hicho, alisema kuwa juhudi za serikali za kupambana na dawa za kulevya, yanahitajika kuungwa mkono na kila mmoja kwani jamii imejisahau na kuwaachia wale ambao wamekumbwa na janga hilo kijipambania wenyewe,hivyo na kujikuta serikali inatumia gharama kubwa kupambana na wahalifu.
Mongela alisema kuwa jamii kubwa bado inafikra dhoofu ikidhania kuwa inaposikia neo mamlaka wanadhani ni waondiyo wanahusika badala yake wanatakiwa wabadilike na kutambua kuwa vita hiyo ni ya taifa zima
''Hakuna sababu ya kujenga shule,vyuo,miundombinu halafu watoto wetu wawe mateja ni kazi bure,tuungane pamoja kupambana na vita hii na Mungu atatusaidia na atatubariki''alisema mongela''
Kwa upande wake Dkt. Kamishna Peter Mfisi alitoa wito kwa jamii kwa ujumla huku akiwataka wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili mema, ikiwemo kuwa nao karibu na kuwasikiliza,huku akiwataka vijana kujiepusha na makundi hatarishi yanayoweza kuwaingiza kwenye matumizi ya sigara ,bangi,ugoro pombe ,shisha au bangi ambavyo watumiaji wengi wa heroin wanakiri walianza navyo.
Aidha Dkt.Mfisi aliitaka jamii kutambua kuwa mirungi haiongezi ufanisi kazini ,ufaulu katika masomo wala nguvu za kiume badala yake vijana wazingatie stadi za maisha na kuepuka kutumia dawa za kulevya kwani ni hatari kwa maisha yao
''Alisema kuwa Mtumiaji anapoacha kutumia heroin hupatwa na arosto,yenye maumivu makali ,homa,kuharisha,kizunguzungu,na kichefuchefu ambavyo hudumu kati ya masaa 48-72,ambapo hupunguza kasi ya utendaji kazi katika mfumo wa ufahamuna kuathiri umakini hivyo kuweza kusababisha ajali,hupunguza nguvu za kiume,na husababisha ugumba''
Kwa upande Dkt.Jesca Temu anayehusika kuwahudumia waraibu wa dawa za kulevya (Methadon) katika hospital ya Mountmeru kwenye cliniki ya Mat, alisema takwimu na hali ya uhalifu na matukio ya usalama barabarani inaonyesha kuwa mka huo kuwa na kesi za mirungi zipatazo 189 zilizoripotiwa ,800 kwa kesi za bangi 169 zilizoripotiwa kwa mwaka 2020,hiyo inachangiwa na hali ya kijiografia ya mazingira,yanayostawisha kilimo cha bangi pia kupakana na nchi Jirani ambapo baadhi ya dawa hizo ni halali.
Temu alisema kuwa mbali na siri ya dawa hizo kuwa na tabia ya kulevya dawa hizo siyo safi katika kazi ya uchumi ya mtumiaji haswa wa kipato cha chini hivyo kuongeza athari zaidi mwilini ambazo zinakuwa na uchafu mwingi zaidi
Aidha amezitaja athari za dawa hizo ikiwemo afya,kuzidiwa na dawa hizo ambazo zinaweza kupelekea kifo kwa mtumiaji,maambukizi ya kifua kikuu,magonjwa ya zinaa,ukimwi na homa ya ini pamoja na magonjwa ambayo siyo ambukizi kama vile akili,shinikizo la damu kiharusi,utimamu wa mwili na utapiamlo.
Athari za kijamii ni pamoja na maadili kuporomoka,tabia mbaya na hatarishi kama vile wizi na lugha chafu, pia ukosefu wa usimamizi na utimamu wa familia pale unapokuta mzazi ni mtumiaji wa dawa za kulevya,kushindwa kumudu familia zao na kuathiri kizazi kijacho,kupotea kwa usalama wa Maisha kutokana na vitendo vya uvunjifu wa Amani.
![]() |
Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo Gerald Musabila Kusaya akizungumza katika mkutano wa uhamasishaji wa upunguzaji wa madahara kwa watumiaji wa dawa za kulevya Mkoani Arusha 15/2/2022 |

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...