Na Mwandishi Wetu
Waandaaji
wa mbio za 20 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon wametangaza vituo
vitatu vya kutolea namba za kukimbilia ambavyo ni pamoja na Dar es
Salaam, Arusha na Moshi.
Taarifa
iliyotolewa jana Jijini Dar es Salaam ilisema zoezi hilo litaanzia Dar
es Salaam katika viwanja vya Mlimani City Jumamosi Februari 19, 2022 na
Jumapili Februari 20, 2022 kuanzia saa sita mchana hadi saa kumi na
mbili jioni kwa siku zote mbili.
“Tunatoa
wito kwa wakazi wa Dar es Salaam ambao wamejisajili wajitokeze kwa
wingi kuchukua namba zao pamoja na vesti za kukimbilia kwa siku mbili
zilizotengwa,” walisema waandaaji hao.
Baada
ya Dar es Salaam, zoezi hilo litahamia Jijini Arusha katika Hoteli ya
Kibo Palace Jumanne Februari 22, 2022 na Jumatano Februari 23, 2022
kuanzia saa nane kamili hadi saa moja kwa siku hizo mbili.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo, zoezi hilo litamalizikia Moshi ambapo namba
hizo zitatolewa katika viwanja vya Chuo Kikuu Cha Ushirika Alhamisi
Februari 24, 2022 kuanzia saa sita mchana hadi saa kumi na mbili jioni,
Ijumaa Februari 25, 2022 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi na mbili
jioni na Jumamosi February 26, 2022 kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa
kumi na moja jioni.
“Washiriki
waliojisajili wanatakiwa kuzingatia muda wa zoezi hili katika vituo
husika ili kuepusha usumbufu na zoezi likishafungwa hakutakuwa na
ugawaji wa namba siku ya mashindano,” walisema waandaaji hao.
Waliongeza
kuwa usajili kwa ajili ya mbio za kilomita 5 bado unaendelea kwa njia
ya Tigo Pesa kwa kubonyeza *149*20# na kwamba usajili pia utafanyika
katika vituo vya kutolea namba.
“Tumefunga usajili kwa ajili ya Km 42 na 21 kwani nafasi zimejaa lakini ule wa Km 5 bado unaendelea,” alisema.
Kwa
upande wake Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Irene Mutiganzi
ambaye bia yake ndio mdhamini mkuu wa mbio hizi, alitoa wito kwa
washiriki wajitokeze kwa wingi kuchukua namba zao tayari kwa mashindano
ya wiki ijayo.
“Waandaaji
wametenga muda wa kutosha wa zoezi hili la kugawa namba kwa Dar es
Salaam, Arusha na Moshi kama wadhamini wakuu tunatoa rai kwa washiriki
wajitokeze mapema ili kuepusha usumbufu dakika za mwisho,” alisema na
kuongeza kuwa wamejiandaa vizuri kuadhimisha miaka 20 ya Kilimanjaro
Marathon.
Wadhamini wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2022 ni Kilimanjaro Premium Lager (Mdhamini Mkuu) Tigo (21km) na Grand Malt (5km).
Wadhamini
wa meza za maji ni pamoja na Absa Tanzania, Unilever Tanzania, TPC
Sugar, Simba Cement na Kilimanjaro Water. Wasambazaji rasmi ni
GardaWorld Security, Keys Hotel, Kibo Palace Hotel, CMC Automobiles na
Surveyed Plots Company Ltd (SPC) na Bodi ya Utalii (TTB).
Katika
hatua nyingine, Kwa mujibu wa waandaaji wa Kilimanjaro Marathon, kwa
mara ya kwanza kutakuweko na maonesho yanayojulikana kama Kili Expo (The
People's Expo) ambapo wadhamini na wadau wengine wa mbio hizo watapata
fursa ya siku tatu za kuonyesha bidhaa na huduma wanazotoa, maonyesho
ambayo yanatarajiwa kufanyika kati ya Februari 24-26, 2022, katika
viwanja vya MoCU.
"Maonyesho
haya pia linakusudiwa kuwapa umma uzoefu wa muda mrefu wa mbio za Kili
Marathon; pia kwa mwaka huu wanaotarajia kushiriki mbio hizo watapata
fursa ya kuchukua namba zao za ushiriki eneo la chuo kikuu cha Ushirika
badala ya eneo la hotel kama ilivyokuwa miaka ya nyuma”, ilisema taarifa
hiyo ya wandaaji.
Mbio
za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, zinatarajiwa kufanyika Jumapili
ya Februari 27, 2022, katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
(MoCU), ambapo zimeandaliwa na taasisi ya Kilimanjaro Company Limited na
kuratibiwa na wadau wa hapa nchini kampuni ya Executive Solutions
Limite
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...