Na Khadija Kalili, Pwani


Kamati ya amani ya Mkoa wa  Pwani  imelaani vikali vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyopelekea mauaji kwa watu wasiokuwa na hatia .

Kauli hiyo ya kulaani vitendo hivyo vya kikatili na mauaji ya watu  katika jamii ambavyo vimeripotiwa na vyombo mbalimbali nchini  Kamati hiyo imesema kuwa hii ni aibu kwa Taifa huku ikisema kuwa wakati Sasa umefika kwa jamii nzima kufanya jitihada za makusudi kyepeuka fedheha hii.

"Jitihada za makusudi zichukuliwe kwa kuanzia katika ngazi ya familia tuanzie chini halafu twende juu kwani katika maisha ya hivi sasa tamaduni zetu zimebadilika kutokana na utandawazi utu wa mtu hakuna Tena, watu hawana hofu ya Mungu Tena hili ni janga hivyo ni wajibu wetu sisi kama.viongozi wa kidini kuungana na kupaza sauti kwani Sasa imetosha"  alisema  Mwenyekiti Mwenza Kamati ya Amani Mkoa wa Pwani  Padri  Benno Kikudo wa Kanisa Katoliki  Parokia ya Tumbi Kibaha.

Padri Kikudo alisema hayo katika Mkutano Maalumu wa ndani  wakati Kamati hiyo ilipozungumza na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge  huku mkutano huo uliohudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama  Mkoa wa Pwani mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Padri Kikudo alisisitiza kwa kusema kuwa  viongozi wa dini wote kwa ujumla wao waungane kwa kutoa mahubiri kwa waamini wao katika  Misikiti na Makanisa watoe mahubiri ambayo yatawskumbusha  jamii kukijenga kizazi cha sasa kiwe chenye maadili na hofu ya Mungu.

Aidha kauli hiyo iliungwa mkono na na Mwenyekiti Mwenza ambaye pia ni  Sheikh WA   Mkoa wa Pwani  Hamisi Mtupa.

Mratibu wa shughuli za Kamati hiyo  Mkoa wa  Pwani Ibrahim Gama alisema kuendelwa  kukithiri  kwa vitendo vya mmomonyoko wa maadili Kamati  hiyo imeshauri  itolewe elimu kwa jamii Ili kumaliza  matukio ya mauaji yanayoendelea.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Pwani  Alhaj Abubakari Kunenge  amewashukuru viongozi hao na kwamba atasimia amani na utulivu ndani ya Mkoa wa Pwani huku akiwataka wakaazi wote Mkoani hapa kuwa na mioyo ya Upendo na kusameheana ikiwa ni pamoja na kuacha roho zenye visasi.

Padri Benno Kikudo wa Parokia ya Tumbi Kibaha akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge akizungumza wakati wa kikao hicho na kueleza kuwa atasimamia amani na utulivu.
Shekhe wa Mkoa wa Pwani Abbas Mtupa akizungumza wakati wa kikao hicho.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...