Kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania Limited leo imekabidhi kisima cha maji kwa wakazi wa Kijiji cha Makangaga na kutoa jumla ya madawati 200 kwa shule za msingi Makangaga na Kiranjeranje zilizopo wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi.
Kampuni hiyo pia imetoa katoni 16 za pedi za keki kwa shule ya sekondari Kiranjeranje, msaada ambao utasaidia kupunguza utoro kwa wanafunzi wa kike ambao hushindwa kuhudhuria masomo wanapokuwa katika mzunguko wa hedhi.
Kisima kilichokabidhiwa kina uwezo wa kuhudumia zaidi ya watu 2,000 na kinatarajiwa kutatua changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama ambayo ilikuwa inawakabili wakazi wa Makangaga waliolazimika kutembea umbali mrefu kutatuta huduma hiyo muhimu.
Akiongea wakati wa kukabidhi misaada hiyo, Mkurugenzi wa Knauf kwa kanda ya Afrika Mashariki Ilse Boshoff, alisema kampuni hiyo ambayo ina migodi ya kuchimba gypsum katika vijiji husika imeamua kutoa misaada kwa wakazi wa vijiji hivyo ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii.
“Mradi huu wa maji siyo tu utaboresha afya za wakazi wa Makangaga bali pia utasaidia shughuli za uzalishaji mali, haswa kwa wanawake na wasichana ambao hawatumia muda mrefu kwenda kutafuta maji na badala yake wasichana watapata muda wa kuhudhuria masomo yao na wanawake kufanya shughuli mbali mbali za kiuchumi,” alisema.
Kwa upande wa msaada wa madawati alisema ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kuaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule hizo mbili
“Tumeamua kutoa msaada wa madawati kwa kuwa tunajua umuhimu wa elimu kwa maendeleo. Kupitia madawati haya tunaamini kuwa wanafunzi wataweza kujifunza katika mazingira bora zaidi,”
Akitoa shukrani zake kwa misaada hiyo, mwenyekiti wa halmashauri ya Kilwa Eston Ngilangwa aliishukuru kampuniya Knauf kwa misaada hiyo na kusema msaada wa madawati umekuja wakati muafaka kwa kuwa shule zilizonufaika zilikuww zinakabiliwa na uhaba wa madawati.
Kuhusiana na mradi wa maji aisema Maji ni uhai, tunawashukuru Knauf kwa kutuletea uhai. Wakina mama na wasichana ambao walikuwa na mzigo wa kutafuta maji kwa ajili ya familia sasa watapata huduma hii muhimu jirani na maeneo wanayoishi,”
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania Limited wakifurahi na wanafunzi wa shuke ya msingi Kiranjeranje iliyopo Kilwa mkoani Lindi muda mfupi baada ya kampuni hiyo kutoa msaada wa madawati 100 kwa shule hiyo. Kampuni hiyo pia ilitoa madawati 100 kwa shule ya msingi Makangaga,kisima cha maji katika Kijiji cha Makangaga na pedi za kike katoni 16 kwa shule ya sekondari Kiranjeranje
Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashari wa Kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania Limited Ilse Boshoff (kati kati) kifurahia jambo na waalimu, wanafunzi wa shule ya Msingi Kiranjeranje pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo muda mfupi baada ya kukabidhi msaada wa madawati kwa 100 kwa shule hiyo
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania Limited wakiongozwa na Mkurugenzi wao wa kanda ya Afrika Mashariki Ilse Boshoff (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, walimu na viongozi wa shule la msingi Kiranjeranje na Makangaga pamoja na viongozi wa elimu wa wilaya ya Kilwa muda mfupi baada ya kuotoa msaada wa kisima, madawati na pedi za kike.
Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashari wa Kampuni ya Knauf Gypsum Tanzania Limited Ilse Boshoff (kulia) akimsiliza mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kiranjeranje Elibariki Kululinda (kushoto) muda mpupi kabla ya kukabidhi msaada wa madawati 100 kwa shule hiyo. Katikati ni meneja rasilimali watu wa kampuni hiyo Rose Mero. . Kampuni hiyo pia ilitoa madawati 100 kwa shule ya msingi Makangaga,kisima cha maji katika Kijiji cha Makangaga na pedi za kike katoni 16 kwa shule ya sekondari Kiranjeranje
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...