Waandaaji
wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon wamewakumbusha washiriki
kuzingatia muda uliotolewa wa kutoa namba za kukimbia huku zoezi hilo
likianza Moshi leo.
Hii
imetokana na baadhi ya washiriki kufika katika vituo vya kutolea namba
wakiwa wamechelewa na kutaka waghudumiwe wakati muda umeshakwisha.
“Tulishuhudia
jambo hili wakati wa zoezi la Dar es Salaam pamoja na Arusha na muda
uliotolewa ulikuwa unatosha kabisa. Lakini baadhi ya washiriki
walichelewa sana na hawakuweza kuhudumiwa kwa sababu tulikuwa tumefunga
tayari,” walisema waandaaji hao.
Waandaaji
hao pia walisisitiza kuwa mara tu muda uliotolewa kwa ugawaji wa namba
kwa mji wa Moshi ukiisha zoezi hilo halitaendelea tena.
Kwa
Moshi namba hizo zitatolewa katika viwanja vya Chuo Kikuu Cha Ushirika
Alhamisi Februari 24, 2022 kuanzia saa sita mchana hadi saa kumi na
mbili jioni, Ijumaa Februari 25, 2022 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa
kumi na mbili jioni na Jumamosi February 26, 2022 kuanzia saa tatu
asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.
Waandaaji
hao walisema mshiriki anaweza kumtuma mwakilishi amchukulia namba
lakini lazima awe na nakala ya kitambulisho na ujumbe wa uthibitisho
aliolipia kutoka Tigo.
“Washiriki
waliojisajili wanatakiwa kuzingatia muda wa zoezi hili katika vituo
husika ili kuepusha usumbufu na zoezi likishafungwa hakutakuwa na
ugawaji wa namba siku ya mashindano,” walisema waandaaji hao.
Waliongeza
kuwa usajili kwa ajili ya mbio za kilomita 5 bado unaendelea kwa
kulipia fedha taslimu katika vituo vya kutolea namba.
Wadhamini wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2022 ni Kilimanjaro Premium Lager (Mdhamini Mkuu) Tigo (21km) na Grand Malt (5km).
Wadhamini
wa meza za maji ni pamoja na Absa Tanzania, Unilever Tanzania, TPC
Sugar, Simba Cement na Kilimanjaro Water. Wasambazaji rasmi ni
GardaWorld Security, Keys Hotel, Kibo Palace Hotel, CMC Automobiles na
Surveyed Plots Company Ltd (SPC) na Bodi ya Utalii (TTB).
Mbio
za Kilimanjaro Premium Lager Marathon, zinatarajiwa kufanyika Jumapili
ya Februari 27, 2022, katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
(MoCU), ambapo zimeandaliwa na taasisi ya Kilimanjaro Marathon Company
Limited na kuratibiwa na wadau wa hapa nchini kampuni ya Executive
Solutions Limited.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...