Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James akizungumza na makarani watakaoshiriki katika zoezi la ukusanyaji taarifa za Anwani za makazi na Postikodi kwa Wilaya hiyo na kuwataka kuwa wazalendo na wabunifu katika zoezi hilo.


MAKARANI Waliochaguliwa na Serikali kushiriki katika zoezi la ukusanyaji wa taarifa za Anwani za makazi na Postikadi Wilaya ya Ubungo wametakiwa kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa weledi na ubunifu utakaosaidia kurahisisha kazi hiyo muhimu kwa watanzania ikiwemo kurahisisha zoezi la Sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka huu.

Hayo yameelezwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James wakati akizindua mafunzo elekezi kwa makarani hao yaliyofanyika katika ofisi za Manispaa Luguruni, Kibamba ambapo amewataka kutumia vyema nafasi hiyo kwa kuhakikisha taarifa ya kila eneo inakusanywa kwa ufanisi na haraka zaidi.

Amesema Wilaya hiyo yenye majimbo mawili ya uchaguzi ina mitaa ipatayo 90 ambayo itapatiwa Anwani za makazi na Postikadi kama Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ilivyoahidi na kudhamiria.

Ameeleza kuwa, kutokana na  ukubwa wa jiografia ya eneo hilo wamewashirikisha makarani hao ili kuongeza nguvu kazi ili kukamilisha kwa ufanisi na haraka.

"Kile kilichoelekezwa kufanyika kiutaalam kifanyike hivyo kwa ufanisi bila kuweka data binafsi, panapohitajika namba za simu, jina la mtu au namba ya NIDA pafanyike kwa ufanisi.....kazi hii ifanyike kwa haraka kabla ya mwezi wa tatu '' Amesema 

Aidha amewataka vijana hao kushirikiana na viongozi na watumishi wa Serikali wakiwemo wenyeviti wa mitaa na watendaji wa Kata ili kuweza kufanikisha zoezi hilo na atakayekwamisha  atachukuliwa hatua za kisheria haraka.

Pia amewataka kushirikiana na jamii watakaofanya nao kazi na kuonesha ushirikiano bila kutoa lugha ya kashfa itakayokwamisha  mchakato huo.

" Ni haki ya mwenyenyumba kudadisi na kuuliza, kuna wahalifu watatumia mchakato huu kufanya uhalifu hivyo wananchi wakiwahoji onesheni ushirikiano." Ameeleza.

Vilevile amewasisitiza uaminifu na ubunifu wa urahisishaji wa kazi kufanya zoezi hilo kwa wakati.

 


sehemu ya makarani wakifuatilia mafunzo hayo.

Viongozi wa ulinzi na usalama wa Wilaya hiyo wakifuatilia mafunzo hayo.





mafunzo yakiendelea.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...