Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James akizungumza na Wenyeviti wa Mitaa, watendaji wa Kata na wananchi wa Kata ya Goba wakati wa uzinduzi wa ukusanyaji taarifa za Anwani za makazi na Postikadi na kueleza kuwa ushirikiano baina ya viongozi, wananchi na makarani utarahisisha mchakato huo, leo Mkoani Dar es Salaam.




MKUU wa Wilaya ya Ubungo Kheri James amesema zoezi la ukusanyaji taarifa za Anwani za makazi na Postikadi lina faida nyingi kwa watanzania ikiwemo kurahisisha mawasiliano, urahisi wa kupata huduma za biashara mtandao, usalama pamoja na kufikiwa kwa urahisi na huduma za kijamii ikiwemo huduma za 'Ambulance' na Zima moto.

Hayo ameyaeleza leo katika Kata ya Goba wilayani humo Mkoani Dar es Salaam wakati akizindua mchakato rasmi wa ukusanyaji wa taarifa za Anwani za makazi na Postikadi kwa Wilaya ya Ubungo na kusema kuwa, wananchi wote wa Manispaa hiyo washiriki katika zoezi hilo la utoaji wa Anwani za makazi ili waweze kunufaika kijamii na kiuchumi pamoja na kurahisisha zoezi la Sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka huu.

"Suala la usalama litaimarika zaidi kupitia zoezi hili vijana wetu wa bodaboda wanabeba abiria na kupita vichochoroni na baadaye abiria kugeuka kuwa mhalifu kupitia anwani za makazi tutakuwa salama zaidi kwa kuwa kila nyumba itakuwa na utambulisho rasmi... katika biashara pia tutakuwa pazuri utaagiza mzigo na kukufikia kwa kutoa Anwani ya nyumba ulipo hata yakitokea majanga ambulance na magari ya zima moto hayatapata shida kufika mahali husika." Amesema.

Amesema, zoezi hilo lifanyike kwa muda maalum kwa kuzingatia weledi na kuwa wa kwanza kimkoa kwa kukamilisha zoezi hilo kwa Mkoa huo.

"Mchakato wa kupata majina ya mitaa na barabara ilikuwa yenu na mmefanikisha hili, kwa sasa Serikali inajukumu la kupata taarifa zenu chache ikiwemo jina lako, namba ya kiwanja kama kimepimwa na namba ya kitambulisho cha utaifa na baadaye namba za Anwani zitabandikwa katika kila nyumba." Amesema.

Kuhusiana na wananchi wanaoishi katika nyumba za kupanga DC Kheri amesema waombe taarifa hizo muhimu kwa wenye nyumba ili kurahisisha zoezi hilo kwa makarani watakaopita kukusanya taarifa hizo.

Aidha amewataka Madiwani, wenyeviti wa mitaa na watendaji wa Kata kusimamia zoezi hilo kwa kupeleka maarifa kwa wananchi ili kurahisisha zoezi hilo la ukusanyaji taarifa.

"Zoezi hili ni operesheni, tutafanya kwa namna maalum na wakati maalum...Kuna zawadi ya shilingi laki tano kwa Mwenyekiti wa Mtaa na mtendaji wa Kata watakaofanya vizuri na kwa muda maalum na kwa watakaofanya vibaya watawajibishwa...., na kwa wakazi ambao hawatakuwa nyumbani waache taarifa hizo kwa watu watakaobaki katika Mji wao tushirikiane katika utekelezaji wa zoezi hili." Amesema.

DC Kheri amesema Serikali ipo tayari kupokea ushauri katika kufanikisha zoezi hilo na haitosita kuchukua hatua kwa yeyote atakayekwamisha zoezi hilo.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ubungo Lucas Mgonja akizungumza wakati wa uzinduzi huo na kueleza kuwa jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita zinatakiwa kuungwa mkono zaidi, leo mkoani Dar es Salaam.


Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James akizindua barabara ya Kinzudi iliyopo Kata ya Goba mkoani Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya uzinduzi rasmi wa mchakato wa ukusanyaji taarifa za Anwani za makazi na Postikadi, leo mkoani Dar es Salaam.






Matukio mbalimbali ya uzinduzi wa mchakato wa ukusanyaji taarifa za Anwani za makazi, Kata ya Goba wilayani Ubungo mkoani Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...