Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
SERIKALI
iko mbioni kuwaondolea karaha ya Ukosefu wa huduma ya usafiri wa mabasi
ya haraka kwa wakazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam ,ifikapo Mwezi
Machi 2023 ,ambapo kwasasa mkandarasi wa ujenzi wa miundombinu amefikia
asilimia 44.4 .
Aidha Wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART ) unakwenda kuboresha miundombinu na Mazingira ya utoaji huduma kwa Kibaha na maeneo mengine ambayo mabasi hayo yameanza kutoa huduma.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Kibaha baada ya kumaliza mafunzo ya wiki
Saba ,kupitia wizara ya uwekezaji, viwanda na biashara chini ya Taasisi
zilizo chini yake Chuo cha elimu ya biashara (CBE ) na SIDO pamoja na
kitengo Cha KAIZEN , Mtendaji Mkuu wa wakala wa Mabasi yaendayo haraka
(DART)Dkt.Edwin Mhede alieleza, wakati wakitarajia ujenzi kukamilika,
Mkandarasi atakapokabidhi na DART watakabidhi kwa mtoa huduma wa mabasi .
Dkt.Mhede
alieleza, ujenzi huo ni ushirikiano wa Taasisi tatu ambapo Wakala wa
barabara TANROADS wakiwa ni wasimamizi wa ujenzi wa miundombinu,UDART na
Wizara mbili ya ofisi ya TAMISEMI na ujenzi ambao ni wasimamizi wa
mradi.
:"Katika mafunzo
tuliyoyapata tunahitaji kuwa na mabadiliko ya kifikra baina yetu DART na
UDART tumekubaliana kufanya maboresho kwenye huduma zetu kuondoa karaha
kwa wateja wetu wakiwemo wa ruti za Kibaha na maeneo mengine" alisema
Dkt.Mhede.
"Tunakiri bado
kuna uhitaji mkubwa wa mabasi kwa mkoa wa Dar es Salam peke yake japo
ina magari mengi binafsi lakini inatoa asilimia 10 pekee ya mahitaji ya
usafiri na asilimia 90 wanategemea usafiri wa umma" alisema Dkt Mhede.
Msimamizi
wa Kitengo cha KAIZEN kutoka Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara
Jane Lyatuu alisema mafunzo yametolewa kwa wiki Saba na yatakuwa
endelevu.
Meneja upangaji
ratiba na udhibiti kutoka kampuni ya mabasi yaendayo kasi UDART Daniel
Madili alibainisha, kupitia mafunzo hayo wanakwenda kufanya maboresho
kwenye huduma zao kwa wananchi.
Baadhi
ya wakazi Kibaha , Loliondo akiwemo Josephine Dachi na Joseph Gabriel
waliipongeza Serikali kwa kuwasogezea huduma ya mwendokasi hadi Kibaha.
Ila waliiomba chini ya DART kuwasogezea huduma hadi Kariakoo kwani wakifika Kimara wanapata shida.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...