Na. John Mapepele
Waziri
wa utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Februari 15,
2022 amekutana na Balozi wa Morocco nchini Mhe. Zakaria Elgoumiri na
kufanya mazungumzo ya kuendeleza sekta za michezo, utamaduni na Sanaa
ambapo Balozi amesisitiza serikali yake ipo tayari kushirikiana na
Tanzania kwa faida ya wananchi wa nchi hizo.
Mhe. Mchengerwa
amesema Serikali ya Tanzania na Morocco zimekuwa na uhusiano mzuri
katika sekta hizo toka muda mrefu hali ambayo imewafanya viongozi
wakuu wa nchi zote kufanya ziara na kubadilishana uzoefu wa sekta
hizo.
Akiwa katika kikao hicho ambacho aliambatana na Katibu Mkuu
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi, Mkurugenzi wa
michezo nchini Yusufu Singo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Michezo (BMT) Neema Msitha wamekubalina na ujumbe wa Mhe. Balozi wa
kuendelea kushirikiana kwenye sekta hizo.
Ameyataja baadhi ya
maeneo ya kipaombele ambayo yanakwenda kufanyiwa kazi kuwa ni ujenzi
na ukarabati wa miundombinu ya michezo, maeneo ya tamthilia na filamu
pamoja na kushirikiana kwa pamoja kuandaa matamasha ya Sanaa na
Utamaduni.
Mhe. Mchengerwa amewakaribisha kushiriki katika
matamasha makubwa ya kihitoria ya Serengeti litakalofanyika jijini
Dodoma Machi 12,2022 na Tamasha la Kimataifa la Utamaduni na Sanaa
Bagamoyo.
Kwa upande wake Mhe. Balozi Elgoumiri amesema Serikali
ya nchi yake inafurahishwa na Sera na diplomasia ya uchumi ya Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu
Hassan hivyo ipo tayari kuendelea kushirikiana na ustawi wa wananchi wa
pande zote mbili.
Ameuomba upande wa Tanzania kukamilisha andiko iliutiaji Saini ufanyike mara moja.
“Tupo
tayari kusaini andiko la kukuza ushirikiano kwenye maeneo
tuliyokubaliana wakati wowote andiko litakapokuwa tayari”. Amesisitiza
Mhe Elgoumiri
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...