SERIKALI imeyafungulia rasmi magazeti ya Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima yaliyokuwa yamefungiwa kwa muda mrefu yamefunguliwa rasmi leo Februari 10, 2022.

Uamuzi huo umetangazwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari na kutoa leseni ya magazeti hayo.

"Agizo la Rais ni Sheria, Leo hii natoa Leseni kwa Magazeti manne ambayo ni Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima. Mama kasema Kazi Iendelee tuanze ukurasa mpya" , amesema Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye.

Akizungumza mara baada ya kupokea leseni za magazeti yake ambayo ni Mwanahalisi na Mseto, Said Kubenea ambaye ni mmiliki wa magazeti hayo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu kwa kufungua ukurasa mpya na vyombo hivyo vya habari huku akisisitiza kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...