CHUO Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam yawajengea uwezo wanachuo wamasomo ya Rasilimali watu na wadau wa rasilimali watu kutoka taasisi mbalimbali.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa mafunzo hayo mtoa Mada, Carl bosser amesema kuwa wasijisikie vibaya kujitathimini pale wanapojijenga kwajili ya kutambulika.
Amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo juu ya wananchuo na washiriki wengine juu ya kuwaimarisha juu ya Chapa binafsi (Personal Branding) ya kile wanachokifanya.
Hata hivyo aliwaeleza umhimu watengeneza chapa binafsi zitakazo wafanya wajulikane zaidi kwa kile wanachokifanya kuliko wanavyojijua wao wenyewe.
Bosser amesema kuwa chapa ni urithi wa maisha ambao kila mmoja anatakiwa kujiwekea katika ufanyaji kazi zake.
Mtoa Mada, Carl bosser akizungumza na wanachuo wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam leo juu ya masuala ya Chapa binafsi (Personal Branding) kwa wadau wa Rasilimali watu na wanachuo wa masomo ya Rasilimali watu wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Mtoa Mada, Carl bosser akizungumza na baadhi ya wanachuo wa masomo ya Rasilimali watu wa Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa mafunzo ya Chapa binafsi (Personal Branding) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wanachuo akitoa ufafanuzi juu ya suala lililojitokeza wakati wa mafunzo ya Chapa binafsi (Personal Branding).
Washiriki wa mafunzo ya Chapa binafsi (Personal Branding) wakimsikiliza mtoa mada, Carl Bosser.
Msheheresaji wakati wa mafunzo ya Chapa binafsi (Personal Branding) akitoa shukurani kwa Mtoa mada mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...