Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara KMC FC dhidi ya Biashara United ya Tarime Mkoani Mara uliopangwa kuchezwa siku ya Ijumaa ya Februali nne katika Uwanja wa Uhuru hapa Jijini Dar es Salaam, umebadilishwa na kwamba sasa utapigwa siku ya  Jumamosi ya Februali tano katika Uwanja wa Azam Complex saa 16:00 jioni.

Kwamujibu wa barua iliyotumwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeeleza kuwa awali mchezo huo ulipangwa kuchezwa siku ya Ijumaa katika uwanja wa Uhuru na kwamba mabadiliko hayo yametokana na kuwepo kwa ukarabati wa miundombinu ya uwanja huo ambao unaendelea kwa sasa.

Aidha barua hiyo pia imeeleza kuwa siku hiyo ya Ijumaa ya Februali nne katika  uwanja wa Azam Complex pia kutakuwa na shughuli nyingine ikiendelea na hivyo kuamua kuusogeza mbele mchezo huo siku ya Jumamosi kwa muda huo huo wa saa 16:00 jioni.

Klabu ya KMC imepokea kwa mikono miwili mabadiliko hayo na kwamba mashabiki ambao walikua wamejiandaa kwa ajili ya kushuhudia burudani safi kutoka kwa vijana wa Kino Boys kwenye uwanja wa Uhuru wajiandae kwa ajili ya kwenda kuwasapoti kwenye uwanja wa Azam Complex kama ambavyo barua ya TPLB Ilivyo elekeza.

“ Tumeona ni muhimu kuwapa taarifa hii mapema mashabiki zetu ilikuepusha usumbufu kwani tunafahamu wengi walijiandaa kuja Uhuru, lakini niwasihi kwamba tujiandae kuwasapoti vijana wetu siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Azam Complex, kama Timu tumejipanga vizuri lakini pia mabadiliko yamekuja kwa wakati hivyo hayawezi kuathiri mchezo wetu kikubwa tujitokeze kwa wingi uwanjani.

Kwa upande wa maandalizi yanaenda vizuri na kwamba wachezaji wanamorali kuelekea kwenye mchezo huo kwa lengo la kuhakikisha kwamba kama Timu tunakwenda kupata ushindi licha ya ushindani mkubwa utakaokuwepo.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thiery Hitimana inaendelea kujifua kwani mchezo huo ni muhimu kwa ajili ya kuhitaji ushindi ili kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC ambapo kwa sasa KMC ipo kwenye nafasi ya 10 ikiwa imeshacheza michezo 13 na kukusanya jumla ya alama 15.

“Kwenye mchezo wetu wa Jumamosi tunahitaji kufanya vizuri, tunakutana na Biashara ambayo nao pia  wanahitaji kupata matokeo ,na ukiangalia kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC tunatofautiana alama Nne, hivyo tutakwenda kupambana ili kuondoka na alama tatu muhimu  siku hiyo kwakuwa mchezo huo upondani ya uwezo wetu lakini pia uimara wawachezaji pamoja na benchi la ufundi tulionao unatupa nafasi hiyo ya kufanya vizuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...