**********************

Na Eleuteri Mangi- WUSM, Dodoma

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul amekutana na Wasanii wa tamthilia ya Huba na kufanya nao mazungumzo juu ya kuboresha kazi zao ili zikubalike ndani ya nchi na kimataifa.

Mazungumzo hayo yamefanyika Februari, 18, 2022 katika ofisi za wizara hiyo zilizopo Mtumba jijini Dodoma ambapo wasanii hao walipata fursa pia kutembelea ujenzi wa jengo jipya la wizara hiyo.

“Asanteni kwa ziara yenu ya kutembelea ofisi zetu hapa Mtumba mji wa Serikali, kwetu sisi ni heshima na faraja. Huo ni uungwana na upendo, sisi tunauthamini jitihada zenu. Hakika tamthilia yenu ya Huba ni nzuri, watu wanaifuatilia sana” amesema Mhe. Gekul.

Akiongea na wasanii hao, Naibu Waziri Gekul amesema kuwa wizara hiyo imekuwa sikivu na inaendelea kusimamia sekta zilizo chini yake kwa kuzingatia maelekezo ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambayo kila mara amekuwa akisistiza Serikali inapaswa kuwa karibu na wadau wake.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Eliya Mjatta amesema tamthilia Huba imekuwa jukwaa la kuitangaza nchi Tanzania zaidi ya miaka sita kimataifa kupitia kisimbuzi DSTV chaneli ya Maisha Magic Bongo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...