Mamlaka
ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imetoa mafunzo ya Siku moja kwa
Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Arusha kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu
utalii wa Urithi wa utamaduni na Mambo Kale
Akitoa mada katika
mafunzo hayo Kamishna Msaidizi Mwandamizi anayesimamia Idara ya Urithi
wa Utamaduni na Jiolojia Eng. Joshua Mwankunda ameeleza kuwa Ngorongoro
ni eneo lenye utalii wa Vivutio vingi ikijumuisha utalii wa mambo kale,
Jiolojia, nyayo za binadamu wa kale, bonde la Olduvai na kambi ya
waanaakiolojia maarufu duniani Dkt. Louis na Merry Leakey.
Eng.
Mwankunda amebainisha kuwa eneo la Ngorongoro ndio sehemu yenye ushahidi
pekee duniani unaolezea historia ya binadamu wa kale duniani pamoja na
gunduzi mbalimbali kwa ufasaha na ushahidi usio na mashaka
“Eneo
la Ngorongoro ndio sehemu yenye gunduzi mbalimbali za historia ya
binadamu, binadamu kusimama na miguu yake miwili, ugunduzi wa fuvu la
binadamu wa kale duniani “zinjathropus” na hata sasa zipo tafiti
mbalimbali zinazoendelea katika bonde la Olduvai" ameafafanua Eng
Mwankunda
Amewaeleza wanahabari hao kuwa kutokana na utajiri wa
rasilimali hizo zilizoipa hifadhi Ngorongoro Sifa mbalimbali duniani za
kiuhifadhi ndio maana UNESCO ilitambua eneo hilo kama urithi wa Dunia.
Kwa
upande Kamishna Msaidizi Mwandamizi anayesemamia Uhusiano wa Umma Joyce
Mgaya ameeleza kuwa Mafunzo kwa wanahabari ni sehemu ya utekelezaji wa
mkakati wa NCAA kutoa uelewa wa bidhaa mbalimbali za utalii zilizopo
katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ili kusaidia kuelimisha jamii juu
ya uwepo wa fursa hizo.
Kaimu Kamishna Msaidizi Mwandamizi- Uhusiano wa Umma NCAA Joyce Mgaya akizungumza na Wanahabari wa Mkoa wa Arusha wakati wa mafunzo kwa wanahabari haoKamishna Msaidizi Mwandamizi (Urithi wa Utamaduni na Jiolojia) Mhandisi Joshua Mwankunda akitoa mada wakati wa mafunzo ya Wanahabari mkoani ArushaWanahabari wakifuatilia mada
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...