Na Khadija Kalili, Pwani
Meneja TARURA Leopold Minja amesema kuanzia Machi Mosi Mkoa wa Pwani utaanza kutumia makusanyo ya maegesho ya magari kwa Njia ya kieletroniki na utaratibu huo utatumika kwa utaratibu wa kisheria kwa kuzingatia kanuni za barabara.
TARURA kwa Mkoa wa Pwani tuna mashine Bagamoyo na kwa.mwezi tunakusanya zaidi ya Mil.1 na kwa miezi sita tayari tumekusanya zaidi ya Mil.17 kwa kupitia mfumo huu hatutegemei mtu kukwepa kulipa ushuru.
Mapato yetu 2020/21 mapato yetu kwa mwaka yalikua Mil 70 lakini kwa mfumo huu mpya tunategemea kukusanya kiasi cha Mil 100.
Alisema kuwa katika eneo la Zegwreni kunajengwa barabara ambayo itahudumia magari mazito, barabara zilizojengwa ni Lulanzi na katika eneo korofi la Kiwanda Cha Viuatilifu.
Pia wanajenga barabara ya kutoka.Muholo kwenda Mbuchi.
Mkuu wa Kitengo TEHAMA TARURA Stanley Mlula alisema.mfumo huu umeondoa ulipaji wa kutumia fedha mbichi ambapo hivi Sasa kutakuwa na siku 14 za kulipa.malimbikizo ya pesa za maegesho pia tozo ya faini imepunguzwa kutoka 50,000 ya zamani ambapo hivi Sasa fine itakuwa ni kiasi cha Sh.10,000 tukikushika ukiwa hujalupa.utalipa deni letu na na hiyo fine pia tumejipanga kushirikiana na Vyombo vya Usalama kama Jeshi la Polisi ili kuweza kulisimamia zoezi hili endelevu.
Ushuru huu utakuwa ukichukuliwa katika maeneo tengefu ya TARURA huku akitoa angalizo kuwa siyo sahihi kwa mtu kutizwa tozo nje ya eneo tengefu (Road Reserve).
Uzinduzi huo umefanywa na Mkuu w Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge huku akianisha faida kubwa ya kwanza ikiwa ni ukusanyaji wa mapato na kutoa taarifa sahihi za mlipaji na kuondoa uwezekano wa upotevu wa makusanyo ya ushuru wa maegesho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...