Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 45 ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika hafla iliyofanyika katika kiwanja cha Polisi Chalinze , Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani akiurahia jambo wakati wa maadhimisho ya miaka 45 ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika hafla iliyofanyika katika kiwanja cha Polisi Chalinze , Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Na Khadija Kalili, Chalinze
RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutumia nafasi ya uchaguzi wa ndani wa chama unaotarajiwa kufanyika mwezi Aprili mwaka huu kwa kuchagua viongozi watakaosaidia kujenga na kukilinda chama.

Dkt. Kikwete amesema hayo leo alipokuwa mgeni rasmi katika kuelekea maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM katika hafla iliyofanyika katika kiwanja cha Polisi Chalinze , Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Dkt. Kikwete amesema kuwa ni vyema wanachana wa CCM kuchagua viongozi ambao watakua wakisikiliza kero za wananchi na kuzitatua, pia wanapaswa kuchagua viongozi ambao watakua na utaratibu wa kukaa na kujadili masuala ya chama ndani ya Kamati ya siasa na kuyapatia utatuzi tofauti na jinsi ilivyo sasa kwani utaratibu hata wa kuweka bendera za wajumbe wa mitaa umekufa huku akitolea mfano kuwa hata hapo uwanjanai hakuna bendera za CCM.

"Kawekeni mikakati ya kutoka hapa tulipo na kwenda mbele natoa ombi maalumu mkatumie vizuri nafasi hii ya uchaguzi wa ndani ya CCM ili tupate viongozi wazuri watakaosaidia kujenga na kuimarisha, kujenga na kuweka mshikamano baina ya chama na serikali yetu tukatae watakaosababisha migogoro ndani ya Chama ,tuepuke mifarakano kwakuto changia viongozi wanaotafuta madaraka kwa sababu ya kujinufaisha wenyewe, na siyo kwa ajili ya chama chetu maana kuna watu wengine wanakuja katika chaguzi huku wakiwa na sababu zao wenyewe" alisema Rais Mstaafu Dkt. Kikwete.

"Mkiona mtu anakuja kwa njaa na maneno ya kutaka mfarakane huyu anashida yake siyo ya chama mkiona watu wa hivyo achaneni nao wanaokuja kwa ajili ya kujijenga wenyewe." Alisisitiza Dkt. Kikwete.

Dkt. Kikwete amewataka wanancha hao kutumia siku ya maadhimisho haya kwa kutafakari na kutathmini chama kililotoka, kilipo na kinakokwenda, huku akisisitiza viongozi wa Jumuiya zote kukumbushana majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuimarisha chama.

Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Bagamoyo Sharifu ambaye ni mwenyeji wa maadhimisho hayo kimkoa akatoa salaam katika sherehe hizo ikiwa ni pamoja na kuomba serikali kuridhia Chalinze kuwa wilaya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...