Na Khadija Kalili ,Pwani

RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan amefungua  rasmi Shule Cha Kimataifa ya siasa itakayofahamika.kwa jina la Mwalimu Nyerere ufunguzi uliofanyika katika eneo la Chang'ombe  Kata ya  Kwamfipa Halmashauri ya Kibaha Mjini Mkoani Pwani.


Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa leo historia ya nchi imeandikwarasmi kwa ufunguzi wa Shule hiyo ya Mwalimu Julius Nyerere ambayo imejengwa kwa ushirikiano wa  pamoja na vyama marafiki sita ambao wote wameunganisha mawazo na kutimiza lengo la kuwa na Shule ya Uongozi .

 Alisema kuwa anaimani kubwa Chuo hiki kitatoa fursa ya kuwapika kiuongozi vijana ambao kwa sasa wamekua wako nyuma katika masuala ya kisiasa hivyo ni muhimu wakajengewa uwezo.

Ameisisitiza vijana zaidi ndiyo wawekewe mkazo katika kuwapa elimu ya uongozi wa Siasa Ili waweze kuja kuwa viongozi madhubuti katika miaka ijayo.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo alisema kuwa Shule hiyo  Ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 200 kwa wakati mmoja  na wataanza kutoa mafunzo rasmi ifikapo  Machi mwaka huu   , alisema kuwa  Shule hiyo  mahitaji yote muhimu .

Rais Samia ametoa pongezi kwa viongozi waasisi walioweka wazo lao la kujenga  Shule   ya Mwalimu Julius Nyerere ambao ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete , Jacob Zuma aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini kwa kupitia Chama Cha (ANC),na Rais wa Msumbiji Philip Nyusi kupitia Chama Cha (FRELIMO) pia amekishukuru Chama Cha Kikomunisti Cha China kwa Msaada  wa ujenzi wa Shule.
 
Mwakilishi kutoka katika Chama Cha SWAPO  Sofia Chinengwa alisema kuwa  tylikuwepo hapa kwa ajili ya kuweka jiwe la ujenzi na Hatari Rais Joseph Pombe Magufuli Mungu ampumzisha Amina,sisi watu wa Namibia tunamtakia heri na nguvu rais Samia Suluhu Hassan Leo tunakwenda kuandika historia kubwa ya mapindu Kusini mwa Afrika na watu wake kuhakikisha wanaondokana na ukoloni .

"Kwa niaba ya serikali tangu na  Chama Changu Cha SWAPO natoa shukrani zangu kwa Chama Cha Kikomunisti kwa kuhakikisha njozi ya kujengwa kwa Chuo hiki Cha Siasa kimejengwa kwa kupitia Shule hii itakua ni muhimu kuendeleza historia ya namna ukombozi ulivyopatikana Kusini mwa Afrika" alisema Chinengwa.

Shule hii itakuwa ni sehemu ya kuendeleza mshikamano na nchi nyingine  duniani ambazo zilichangua kwa kupata uhuru Kusini mwa Afrika.

Katibu kutoka Chama Cha ZANUPF Mbopo Dokta aliyesema kuwa alikua nchini 1968 alipokuwa na umri wa miaka 16 ambapo alikuja kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya ukombozi huku akisema.kwamba amefurahi kupata fursa ya kushuhudia ufunguzi wa Chuo hiki .

Shule hii itakua ni sehemu ya kuondoa mawazo mbalimbali ambayo sisi waafrika tumepanga kuyaondoa na kupitia Chuo hiki tutaonhesha dhamira yetu ya kuondokana na ukoloni"  alisema.

Chuo hiki kimekuja katika wakati muafaka kabisa kwanza itakua ni sehemu ya mifumo ya siasa inayoihusu bara la Afrika, itakua ni sehemu ya kufanya utafiti katika suala la utamaduni, na kupitia Chuo hiki tunazialika nchi nyingine kutoka kila kona ya dunia waje kujifunza .

Mwakilishi kutoka Chama Cha ANC Chama Tawala Cha Afrika  Kusini Sibagonile Basani wengine ni
 Manueli Domingo  Agusto  mwakilishi wa Chama Cha  MPLA, Fransisco Mkatlea aliyewakilisha Chama Cha FRELIMO Cha  Msumbiji.

"Ufunguzi huu wa Chuo unaunganisha uhusiano wetu wa vyama rafiki na vyama vyote vilivyoshiriki katika ukombozi wa nchi zilizopo Kusini mwa Afrika Tanzania ilikua sehemu salama walipoanzisha harakati zanukomvozi wa watu wa Kusini mwa Afrika FRELIMO inaona Chuo hiki ni sehemu muhimu sana Kwa kuandaa viongoy ambao wataweza kuwa viongozi wa vyama vyetu katika mazingira ya Sasa ya ulimwengu na ushiriki wetu wa kwanza katika kushiriki Ili kuhakikisha malengo ya Chuo hiki yanatimia FRELIMO tunakipongeza sana Chama Cha Mapinduzi (CCM),kwa kukamilisha ujenzi huu pia tunakipongeza Chama Cha Kikomunisti Cha Cha China.
Mwakilishi wa NPLA 

Ufunguzi huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja  na Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Philip Mpango, Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Mohammed Shein ,Katibu Mkuu Daniel Chongolo, wajumbe wa Halmashauri Kuu Taifa , Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, Makatibu Wakuu wastaafu Philip Mangula  Bashiru Kakuru.

Chuo hiki kimejengwa kutokana na mawazo ya vyama sita marafiki  vya siasa vilivyoungana katika kupigania uhuru Kusini mwa Afrika ambavyo ni ANC,NPLA,ZANUPF, FRELIMO,SWAPO na CCM.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...