Na Muhidin Amri, Madaba
MKUU wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge,ameagiza wakala
wa huduma za Misitu Tanzania(TFS)kutumia mvua zinazoendelea kunyesha
kuongeza kasi ya kupanda miti katika maeneo ya wazi yaliyoathiriwa na
shughuli za kibinadamu katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
Ibuge ametoa agizo hilo jana, wakati akizundua mpango wa upandaji miti
kimkoa uliofanyika katika kijiji cha Mwande kata ya Mateteleka
Halmashauri ya Madaba wilayani Songea.
Aidha Brigedia Ibuge,amewaonya wananchi kuacha tabia mbaya ya kuchoma
kwa makusudi miti inayopandwa na Serikali kupitia wakala wa huduma za
misitu(TFS)kwa kuwa hiyo ni sehemu ya miradi inayoliingizia Taifa fedha
nyingi.
Alisema,kuchoma moto kwa makusudi mashamba ya miti ni ushamba na kamwe
Serikali haitawavumilia hata kidogo watu hao kwa sababu Serikali
inatumia fedha nyingi kuandaa mashamba hayo na amewataka wananchi,
kuheshimu uwekezaji huo.
Katika hatua nyingine,Mkuu huyo wa mkoa ameipongeza TFS kwa kupanda miti
laki saba tangu mvua za masika zilipoanza kunyesha katika maeneo
mbalimbali ya mkoa huo.
Hata hivyo, ameomba kazi hiyo iwashirikishe wananchi na kutoa ushauri
kuhusu miti sahihi inayopaswa kupandwa, badala ya kuacha wananchi
wanapanda miti holela na matokeo yake kukauka kutokana na kupandwa
sehemu zisizo sahihi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa,Serikali haiwezi kutekeleza kila jambo pekee
yake, bali wananchi ni muhimu washirikishwe na washiriki katika shughuli
zote za maendeleo kwani hatua hiyo itasaidia kulinda miradi hiyo kwa
kuwa wataiona ni yao.
Akizungumza na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Madaba wakiongozwa
na Makamu Mwenyekiti Olaph Pili Mkuu huyo wa mkoa alisema, maeneo mengi
ya Madaba yana changamoto ya ukataji na uchomaji moto miti,hivyo ni
lazima kupanda miti kwa wingi.
Mkuu wa mkoa ameitaka Halmashauri ya Madaba, kutunga na kutumia sheria
ndogo zinazomtaka kila mwananchi katika eneo lake kuhakikisha anapanda
miti na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaofanya shughuli kwenye
vyanzo vya maji na maeneo yasioruhusiwa.
Kuhusu wananchi waliotoa maeneo yao ya kilimo na kuwekwa mipaka
(Bikoni) alisema, ni vyema Halmashauri kufanya tathimini ya kina kujua
watu wangapi walioathirika ili wapewa maeneo mengine kwa ajili ya
kuendelea na shughuli zao.
Amewaonya wananchi walioondolewa katika maeneo ya hifadhi kufanya
shughuli zao kutodai fidia yoyote kwani wao ndiyo wenye makosa kwa
kuingia na kuvamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya vyanzo vya maji.
Kamanda wa Wakala wa huduma za Misitu Tanzania(TFS)Kanda ya Kusini
Manyisye Mpokigwa alisema,TFS ina jukumu la kuhakikisha vyanzo vyote vya
maji vinalindwa kwa kushirikiana na wadau wengine wakiwamo mamlaka na
wakala za maji(Ruwasa) kwa kupanda miti katika maeneo yote
yaliyoathirika na shughuli za kibinadamu.
Naye Meneja wa shamba la miti Wino Glory Kasmir alisema, hadi sasa
wamefanikiwa kupanda miti laki saba katika vijiji na maeneo ya ofisi
za Serikali kwa ajili ya kurudisha maeneo yaliyoathirika katika hali
yake ya asili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...