Na; Mwandishi wetu - Nzega
Wakulima katika Halmashauri ya mji wa Nzega Mkoani Tabora, wameonesha kuwa tayari na kutoa ushikiano kwa ujenzi na ukarabati wa mradi wa kilimo cha Umwagiliaji Idudumo unaofadhiliwa na Serikali kwa silimia mia.
Wakiongea kwa nyakati tofauti katika makabidhiano ya eneo la kazi katika skimu hiyo, Bw. Pascal Maganga ambaye ni mkulima wa zao la mpunga katika skimu hiyo alisema, ujenzi na ukarabati wa miundombi katika skimu hiyo utasaidia wakulima kulima zaidi ya mara moja katika misimu tofauti ya mvua, tofauti na sasa ambapo ukosekanaji wa miundombinu unapelekea mashamba kujaa maji na kutokulima kwa wakati na kuweza kuleta madhara kwa mazao.
“Naamini kuwa baada ya ujenzi na maboresho haya, kwa heka awali mkulima kama alikuwa anapata gunia thelathini (30) ila baada ya maboresho haya tutavuna zaidi .” Alisee Mkulima hiyo.
Akiongea wakati wa makabithiano hayo, Meneja mradi huo Mhandisi Juma Kibori kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji alisema, eneo la skmu hiyo ya kilimo cha Umwagiliaji yenye ukubwa Hekta 300, na kujikita zaidi katika kilimo cha mpunga lenye chanzo chake cha maji ya Bwawa la Idudumo, lilikuwa likitumia njia za asili na sasa itajengewa mfereji mkubwa wa kupeleka maji mashambani wenye urefu wa mita 1500, vigawa maji sita, makaravati matano na mifereji ya upili yenye urefu wa mita zaidi ya mia sita.
Aliendelea kusema kuwa, awamu hiyo ya kwanza ya ujenzi na ukarabati wa skimu hiyo utakaogharimu zaidi ya shilingi milioni 700, unaotegemea kuchukua miezi nane, utaboresha miundombinu na kusaidia wakulima kuwa na kilimo cha uhakika.
Mhandisi Mwinchuma Tengeneza (kulia) akimkabidhi kablasha la
eneo la kazi ya Ujenzi na Ukarabati wa
miundombinu, katika skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Idudumo mwakilishi wa
Kampuni ya Ujenzi ya Explicit Main Constructors Ltd Bw. Basil Clement
(kushoto).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...