Mkuu wa Mkoa Pwani Alhaji Abubakar Kunenge amesema kuwa ni wajibu wa Serikali kupanga miji huku lengo kuu likiwa ni katika kuvutia wawekezaji kuwekeza Mkoani hapa.
RC Kunenge alisema hayo leo wakati alipokuwa Mwenyekiti wa kikao Cha Baraza Biashara katika kikao kilichofanyika.kwenye Ukumbi uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani nakuhudhuriwa na Wakurugenzi kutoka katika Halmashauri Wakuu wa Wilaya, wafanyabiashara pamoja na Wakuu wa Idara mbalimbali ndani ya Mkoa wa Pwani.
"Tumejipanga kupanga maeneo yote ya Ili tuweze kwenda sambamba katika mpango mzima wa kupanga miji Ili iweze kufahamika vyema yalipo maeneo ya viwanda na makazi ya watu Ili kuweza kuzikwepa atharizinazoweza kuletwa na kuwepo kwa viwanda katika maeneo ya makazi ya watu" aliseme RC Kunenge.
Kunenge aliongeza kwa kusema kuwa"Tutayapanga maeneo tuliyonayo Ili yaweze kukaa katika mpangilio mzuri na itakayowavutia wawekezaji pamoja na kutunza mazingira.
Alizungumza hayo leo asubuhi katika mkutano wa baraza la uwezeshaji la wafanyabiashara.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibaha Mhandisi Mshamu Munde alisema alichangia mada kuhusu suala la upimaji alisema kuwa tayari wamepata Bil.1.5.88 kwa ajili ya utambuzi wa maeneo ya viwanja.
"Tumekamilisha kupima katika eneo la kidimu na Lulazi yaliyopo katika eneo la Kata ya Pangani Kibaha Mkoani Pwani huku lengo letu likiwa kukamilisha viwanja 20,000"alisema Mkurugenzi huyo.
Wakati huohuo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Mheshimiwa Ramadan Possi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...